HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 25, 2018

KUELEKEA UCHUMI WA KATI, BAOBAB WAFUNGUA KIWANDA CHA UTENGENEZAJI MITA ZA LUKU


Mtaalamu wa IT wa Kiwanda hicho,Isaya Hezron akijibu maswali ya waandishi wa hari leo jijini Dar es Salaam. 

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
WAZIRI wa nishati mh. Menard Kalemani leo Machi 24 ametembelea kiwanda kipya cha utengenezaji wa mita za luku cha Baobab Energy System Tanzania (BEST) kilichopo Goba jijini Dar es Salaam.

Kalemani ameeleza kuwa lengo la kutembelea kiwanda hicho ni kukagua na kujiridhidha ili kutoa zuio la kuagiza mita nje ya nchi.

Aidha Kalemani amefurahishwa na utendaji kazi wa kiwanda hicho ambacho huzalisha mita 38 elfu kwa mwezi na mita 56 elfu kwa mwaka ambayo ni zaidi ya mahitaji ya TENESCO na REA ambao huhitaji mita 20 elfu pekee kwa mwezi hivyo wamejiridhisha na uwezo wa kiwanda na kutoa miezi mitatu ya matazamio baada ya hapo hakuna mita zitakazoagizwa nje ya nchi.

Pia Kalemani ameeleza sababu za kuanzishwa viwanda hivi ni kwenda sambamba na uchumi wa viwanda, urahisi katika upatikanaji wake na ubora.Pia ameeleza faida za mita hizi ambazo ni pamoja na kuongeza mapato kwa TANESCO, kudhibiti wizi wa umeme kwa asilimia 90 kwa kuwa mita hizi ni za kisasa, kuokoa umeme wa asilimia 38 unaopotea kila siku na kuondoa kero kwa wateja.

Amewataka wawekezaji wawe na ushindani kwa kufungua viwanda kama hivi maeneo mengine ili kurahisisha usafirishaji kwani hadi sasa ni viwanda viwili tuu ndivyo vinavyozalisha mita hizi na kuwataka waendeleze viwanda hivi. Pia ametoa rai kwa TANESCO na REA kufanya kazi kupitia teknolojia hii ili kuepukana madeni na mizigo na amewataka wananchi kuwekeza kwenye miundombinu ya nishati kama Baobab.

Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo Hashim Ibrahim amemshukuru waziri na kueleza kuwa wanaunga mkono sera ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda, na kufafanua kuwa kiwanda hiki kilianza kufanya kazi Machi 15 mwaka huu na walianza kama wasambazaji wakishirikiana na TANESCO kwa zaidi ya miaka 10 na amehaidi kufanya kazi na TANESCO katika upatikanaji, usambazaji na uhifadhi kama walivyokuwa wanafanya kazi miaka iliyopita.

Mtaalamu wa IT wa Kampuni hiyo Isaya Hezron ameeleza kuwa wameungana na kampuni ya EDMI ya Singapore ili kuweza kurahisisha huduma kwa wateja wake aidha ameeleza kuwa mita hizo hufanyiwa matengenezo pindi zinapoharibika tofauti na mita nyingine pia mita hizi ni zilezile zinazohitajika na TANESCO kwa matumizi ya nyumbani na viwandani.

 Waziri wa Nishati,Menard Kaleman azungunza na akifafanua jambo mble ya wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza mita za luku cha Baobab Energy System Tanzania (BEST) kilichopo Goba jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Mita za Luku, Hashim Ibrahim(kulia) akitoa maelezo mafupi mbele ya Waziri wa Nishati,Menard Kaleman leo alipotembelea kiwanda hicho.
 Waziri wa Nishati,Menard Kaleman (wakwanza kushoto) akiwa ameambatana na viongozi mblimbli wakiwasiri katika kiwanda cha kutengeneza mita za luku cha Baobab Energy System Tanzania (BEST) kilichopo Goba jijini Dar es Salaam.
Wafanyazi wakiwanda hicho wakiendelea na kazi.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad