HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 5, 2018

​SERIKALI YATOA BIL. 1.4 KUBORESHA VITUO VYA AFYA RUANGWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 kwa ajili ya uboreshaji wa vituo vitatu vya afya katika wilaya Ruangwa mkoani Lindi.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Machi 04, 2018) wakati alipotembelea kata ya Mandawa kwa ajili ya kukagua mradi wa uboreshaji wa kituo cha afya cha kata hiyo.
“Serikali imeamua kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.”
Waziri Mkuu amesema kati ya fedha hizo sh. milioni 400 kwa ajili ya kituo cha Mandawa, sh. milioni 500 kituo cha Mbekenyera na sh. milioni 500 Nkowe.
Amesema uboreshaji huo unahusisha ujenzi huo chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, wodi ya mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume na chumba cha kuhifadhia maiti.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.
Pia Waziri Mkuu amekabidhi gari la kutolea huduma za afya vijijini. Gari hilo linauwezo wa kutoa huduma za afya kama Zahanati. 
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameshiriki katika zoezi la ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya  ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Matambarare.
Amesema kata hiyo yenye vijiji vinne ilikuwa haina shule ya sekondari, hivyo kusababisha wanafunzi kutembea umbali wa kilomita tano kwenda kusoma kwenye shule za kata nyingine.
 Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akichanganya udongo wa tofali, wakati akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale, Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akiweka udongo wakati akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale, Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018
 Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akifyatua tofali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale, Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad