HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 5, 2018

WAZIRI UMMY MWALIMU, BALOZI WA PALESTINA WAINGIA MAKUBALIANO KUSHIRIKIANA SEKTA YA AFYA

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalim pamoja na Balozi wa Taifa la Palestina nchini Tanzania Hazem Shabat wametia saini ya mkataba wa ushirikiano kwenye sekta ya afya.
Kupitia mkataba huo Taifa la Palestina pia litasaidia katika kuleta madaktari kwa ajili ya kutibu magonjwa yakiwamo ya uti wa mgongo ambapo madaktari wao na wa Tanzania watafanya kazi pamoja ya kutoa huduma za afya.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Waziri Mwalim amesema kuwa wanatambua kuna changamoto katika kutibu baadhi ya magonjwa nchini, hivyo madaktari bingwa wa Palestina na madaktari bingwa waliopo nchini watatumia fursa ya mkataba huo wa ushirikiano katika kutoa huduma za tiba kwa Watanzania.
Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano,chini ya Rais, Dk.John Magufuli imekuwa na jitihada  mbalimbali za kuboresha sekta ya afya lakini mkataba uliotiwa saini leo unatoa fursa ya kuimairisha pia utoaji wa chanjo na dawa.
Amesema mkataba huo umejikita kwenye maeneo mbalimbali na baadhi ni kusaidia katika kutoa huduma za afya, kusaidia upatikanaji wa dawa, kuimarisha eneo la Tehama ili kuboresha huduma hasa kwa kuzingatia teknolojia ya habari na mawasiliano itasaidia kuimarisha mfumo wa kutunza kumbukumbu za sekta ya afya.
“Kupitia mkataba huu kuna kipindi Taifa la Palestina , madaktari wetu watakwenda huko na madaktari wa huko nao watakuja nchini kwetu kwa lengo la kubadilishana uwezo wa kitaalamu,”amesema Waziri Mwalim.
Amefafanua  kutokana na mkataba huo, anaamini itakuwa fursa nzuri ya kuiomba Palestina kuwekeza katika ujenzi katika viwanda vya dawa na kueleza Tanzania imekuwa ikiagiza dawa kutoka nje kwa asilimia 80, hivyo viwanda vitakapojengwa nchini itasaidia dawa kupatikana nchini.
“Hivyo nimewaalika wenzetu hawa kuwekeza kwenye eneo la dawa na chanjo kwa ajili ya kusaidia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa dawa ambazo kwa sehemu kubwa zinatoka nje ya nchi yetu,”amesema.
Kwa upande wa Balozi wa Taifa la Palestina nchini Tanzania, Hazem Shabat amesema lengo lao ni kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya afya na kuongeza yote ambayo wamekubaliana wataanza kuyashughulikia haraka.

“Taifa la Palestina litahakikisha linaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha sekta ya afya na makubaliano ambayo tumeingia leo ni hatua ya kuanza kwa utekelezaji wa yale ambayo tumeamua kushirikiana,”amesema Balozi Shabat.

 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimuakibadilishana mikataba na Hazem Shabat Balozi Palestina Nchini Tanzania baada ya kutiliana saini kwa ajili ya  ushirikiano kati ya Tanzania na Palestina katika sekta ya afya, Hafla ya kutiliana saini imefanyika kwenye Ofisi Ndogo ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jijini Dar es salaam. Kushoto ni Msaidizi wa Kwanza wa Balozi wa Palestina Derar Ghannam.
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimuakizungumza na mara baada ya kusaiini mikataba ya ushirikiano katika sekta ya Afya  kati ya Tanzania na Palestina kushoto ni Hazem Shabat Balozi Palestina Nchini Tanzania.
 Hazem Shabat Balozi Palestina Nchini Tanzania akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mikataba hiyo, Kulia ni Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. 
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  na Hazem Shabat Balozi Palestina Nchini Tanzania wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mikataba hiyo kushoto ni Msaidizi wa Kwanza wa Balozi wa Palestina Derar Ghannam.

Baadhi ya maofiza kutoka wizaya ya Afya wakiwa katika hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad