HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 1 February 2018

TATIZO LA MAJI LINDI MJINI KUBAKI HISTORIA.

Na Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amefanya ziara kutembelea mradi wa maji wa Ng'apa  Mkoani  Lindi  wenye thamani ya  Euro milioni 11.7 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali. 

Profesa Mkumbo amesema  kuwa wananchi  wa Lindi wanaanza  kupata huduma ya maji   leo Februari mosi huku   kazi ndogondogo zilizobaki katika mradi huo zikiendelea kukamilishwa.

Akifafanua amesema kuwa mradi huu unatarajia kuzalisha kiasi cha lita milioni 7 za maji  kwa siku kiasi ambacho kitakidhi mahitaji ya maji   Lindi mjini kwa sasa na kuchochea ukuaji wa uchumi  na uzalishaji, Aidha mahitaji  ya maji ya mji huo ni kiasi cha lita milioni 5 kwa siku .

“ Mamlaka ya maji na usafi wa  mazingira Lindi (LUWASA) itafanya kazi ya ukarabati wa miundombinu iliyopo pamoja na kuongeza mtandao katika vitongoji ambavyo havina mtandao wa mabomba “ Alisisitiza Profesa  Mkumbo. 

Aidha,  Profesa Mkumbo ametoa wito kwa wananchi Mkoani Lindi kulinda miundombinu ya maji na  kulipa ankara za maji waliyotumia ili huduma hiyo iwe endelevu na ichangie katika kuleta maendeleo.

Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeweka mkazo katika kuimarisha huduma za jamii hasa zile zinazowagusa wananchi wanyonge ikiwemo upatikanaji wa maji safi na Salama  kwa wananchi wake kote nchini hali inayochochea kasi yautekelezaji wa miradi ya maji katika Mikoa na Wilaya mbalimbali hapa nchini.

Mradi huo umetekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji  ambapo mkandarasi ni Kampuni ya  OIA ya nchini india.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji  Profesa Kitila Mkumbo akisikiliza maelezo kutoka  kwa mshauri muelekezi  wa mradi  maji wa Ng'apa  Mkoani Lindi bw.Colman Ngainayo (wakwanza kulia), wakati  wa ziara  yake yakukagua mradi huo wenye thamani ya  Euro milioni 11.7 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali, mradi huo utawanufaisha wakazi wa Lindi mjini kuanzia leo Februari mosi, kushoto ni meneja wa mradi huo kutoka Kampuni ya OIA ya nchini india
 Bw. Rajeev Rai.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la mradi  wa maji wa Ng'apa  Mkoani  Lindi  utakaowanufaisha wakazi wa Lindi mjini kuanzia leo Februari mosi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad