HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 8, 2018

SINE TAMER YATILIA MKAZO AGIZO LA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI

 Rais wa Sine Tamer Tim Chima (wa kwanza kulia) akiwa sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanfas Ndaki Munyeti pamoja na Mkurugenzi wa Sine Tamer Tanzania Dotto Ibambasi kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla maalumu ya kukitambulisha kifaa maalumu cha kudhibiti umeme.

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
Kampuni ya Sine Tamer imedhamiria kuhakikisha inatilia mkazo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli la kuwa katika uchumi wa kati wa  viwanda kwa mwaka 2025.

Hayo yamesemwa katika mkutano na wadau mbalimbali wa masuala ya nishati hususani katika viwanda, makampuni binafsi, mahospitali, mabenki na mashirika mbalimbali.

Mkurugenzi wa Sine Tamer nchini Tanzania Dotto Ibambasi amesema ndani ya miezi 7 tokea Juni 2017 wameweza kusambaza kifaa hicho kwa hospitali ya Muhimbili na wameweza kuonyesha mafanikio baada ya kuanza kukitumia ikiwemo kupungua kwa gharama za ufundi wa vifaa vilivyokuwa vinaharibika mara kwa mara.

"Kifaa hiki kimeweza kutumika katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili na wameonesha mafanikio makubwa sana baada ya kuanza kukitumia kifaa hicho kwani wameweza kupunguza gharama za ufanyaji wa ukarabati wa mara kwa mara,"amesema Ibambasi.
Akielezea kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda, Ibambasi amesema kuwa mikakati yao mikubwa ni kuhakikisha wanashirikiana na viwanda kwenye matumizi ya kifaa hicho kwa ajili ya kusaidia upunguzaji wa gharama za matumizi ya ukarabati wa mitambo kwani baadhi ya vifaa vingine hususani Balbu zinaungua kutokana na umeme kuja mchafu.

Ibambasi amesema kuwa mpaka sasa ni kampuni ya NMB imeweza pia kutumia kifaa hicho na wameweza kuona umuhimu wa kifaa hicho ambapo wamekiweka kwenye vituo vyao mbalimbali.

Kifaa hicho kimetambulishwa leo kwa wadau na wameaswa kukitumia ili kuweza kupunguza gharama za ukarabati wa mashine, mashine kuwa sawa pia kupunguza matatizo ya kuhangaika kupata vipuli vya mashine pindi vinapoharibika.
Mkurugenzi wa Sine Tamer nchini Tanzania Dotto Ibambasi akizungumzia kifaa hicho na kuelekezea namna kilivyoweza kusaidia kwenye kudhibiti uharibifu wa vifaa vya umeme pamoja na gharama za matengenezo.
Wadau mbalimbali waliojitokeza katika hafla hiyo.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad