HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 17 February 2018

NAIBU WAZIRI ULEGA AWATAKA WANANCHI MKONO JUHUDI ZA VIONGOZI WAO


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega  akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Maragoro wakati wa ziara yake katika kata ya Vianzi na kuwapongeza kwa ufaulu mzuri wakiongoza kwa kata kwenye matokeo ya darasa la nne na la saba.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega amewataka wananchi wa Kata ya Vianzi kumuunga mkono diwani wa kata hiyo Nassoro Chuma katika kuendeleza miradi mbalimbali ya Kijiji.

Hayo aliyasema wakati wa ziara yake katika jimbo la Mkuranga kwa kutembeklea kaya ya Vianzi na kujionea maendeleo yaliyofanywa na mengine yakiwa katika hatua nzuri ambayo yanasimamiwa na diwani Chuma kwa ushirikiano na viongozi wa vijiji
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega sambamba na diwani wa kata ya Vianzi Nassoro Chuma , Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkuranga Ally Msikamo na mganga mfawidhi wa Zahanati ya Marogoroni Zulfa Makubui wakizundua nyumba ya mganga wakati wa ziara yake katika kata ya Vianzi.

Mbali na ujenzi wa barabara pia tayari wakala wa barabara za vujijini na mijini (TARURA) wameshaanza mradi wa ujenzi wa daraja la kijiji cha Sangatini utakaogharimu kiasi cha milioni 122. 


Wakati wa ziara hiyo Naibu Waziri Ulenga aliweza kuzindua Zahanati ya Mfuru Mwambao iliyojngwa kwa msaada wa kanisa na kisha kukabidhiwa kwa wanakijiji ikiwa na changamoto ya ukosefu wa nyumba ya mganga na upatikanaji wa dawa kutoka bohari ya dawa ya taifa (MSD).

Pia kweye kijiji cha Marogoro Ulega alizindua nyumba ya mganga na aliweza kwenda kuona ujenzi wa shule ya msingi Sangatini iliyojengwa kwa nguvu za wananchi ikigharimu milioni 13.5 kwa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi moja ya mwalimu, na katika shule ya msingi Marogoro aliweza kutoa kiasi cha shillingi laki tatu (300,000) na mifuko 30 ya saruji kwa ajili ukarabati wa madarasa.

Akizungumza na wananchi mbalimbali Ulega amewataka kulitumia eneo lililokuwa limehifadhiwa kwa muda mrefu na likiwa limetengwa maalumu kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege kwa kuendelea kufanya shughuli zao kijmaii namaendeleo.

Ulega atakuwa na ziara ya siku tatu akitembelea kata mbalimali za jimbo la Mkuranga na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ambapo hilo linmekuwa ni kawaida yake mara kwa mara kukaa na wananchi wake na kuwasikiliza.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akizunumza na wanakijiji wa Mfuru Mwambao wakati wa ziara yake katika kata ya Vianzi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akiweka tofali kwenye kuendeleza ujenzi wa shule ya msingi Msangatini wakati wa ziara yake katika kata ya Vianzi.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akiwa sambamba na diwani wa kata ya Vianzi Nassoro Chuma wakizuru katika shule ya msingi Marogoro wakati wa ziara yake katika kata ya Vianzi.Picha na Emmanuel Massaka

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad