HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 17, 2018

WASHINDI WA SHINDANO LA WATOTO VIBES WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO LEO JIJINI DAR.

Mratibu wa mradi wa Watoto Vibes Malega Wiliiams akitoa zawadi kwa mshindi wa kwanza wa shindano la Watoto Vibes Ibrahim Heri wakati wa utoaji wa zawadi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHINDANO la kusaka vipaji wa watoto lililoandaliwa na asasi ya kiraia Voice of Change Tanzania lililoratibiwa kuanzia mwishoni mwa mwaka jana limehitimishwa leo kwa washindi kupatiwa zawadi zao ikiwemo kuwaendeleza kimuziki.

Hitimisho hilo liliofanyika mbele ya waandishi wa habari washindi hao waliweza kukabidhiwa fedha taslimu mbele ya wazazi wao na waratibu wa shindano hilo kuwaahid kuwaendeleza kimuziki pamoja na shindano hilo likiwa ni ebdelevu kwa mwaka huu kwenda katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Mbeya.

Akizungumza kabla ya kuwakabidhi zawadi zao, Mratibu wa mradi wa watoto Vibes Malega Wiliiams amesema kuwa mradi huu umelenga zaidi katika kuibua buna kukuza vipaji vya watoto wenye tija ya kutaka kuleta mabadiliko chanya katika jamii, kuongeza fursa za ajira na kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika taifa la Tanzania.

Williams amesema kuwa, walengwa wakuu ni watoto wasiozidi miaka 15 kwani watoto wa rika hilo wana hazina, neema na uwezo wa kugusa na kubadilisha maisha ya watu kwa kutumia vipaji vyao ila mara nyingi huwa wanakosa mazingira rafiki, malezi na nafasi ya kufanya kazi zao hivyo huishia kudidimia na kushindwa kutimiza kusudi lao.


"Mashindano haya yanaendeshwa kwa mfumo wa mashindano ya kusaka vipaji ambapo washindi hujipatia zawadi ikiwa ni pamoja na mafunzo katika nyanja ya vipaji vyao, malezi na kurekodi na kutafutiwa fursa za kutumia vipaji vyao.

Jaji Mkuu wa Shinano hilo Bella Kombo ameeleza  kuwa watoto hao walionesha uwezo wa hali ya juu, ushindani mkubwa kiasi kwamba  walikuwa na wakati mgumu wa kuchagua washindi kwani watoto walikuwa wamejiandaa vizuri.


Mshindi wa kwanza aliweza kujinyakulia kiasi cha shilingi laki tano (500,000) mshindi wa pili ni laki tatu (300,000) na wa tatu akipokea laki mbili (200,000).

Shindano la mwaka 2018 linatarajiwa kuanza mwezi wa saba na litakuwa katika mikoa ya Arusha na Mbeya na Wtoto Vibes wanejiandaa na semina kwa wazazi wa sasa na wazazi watarajiwa kuhusu malezi bora kwa mtoto ambapo inatarajiwa kufanyika Machi 26 mwaka huu.

 Mratibu wa mradi wa Watoto Vibes Malega Wiliiams akitoa zawadi kwa mshindi wa pili wa shindano la Watoto Vibes  Ibrahim Urassa wakati wa utoaji wa zawadi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mradi wa Watoto Vibes Malega Wiliiams akitoa zawadi kwa mshindi wa tatu wa shindano la Watoto Vibes Rebbeca Steven wakati wa utoaji wa zawadi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Picha na Zainab Nyamka

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad