HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 23, 2018

WANAVYUO MKOANI TABORA WATAKIWA KUTUMIA NAFASI ZAO KULINDA NA KUHIFADHI MAZINGIRA.

Na Tiganya Vincent

WANAVYUO Mkoani Tabora wameagizwa kuhakikisha kuwa wanatumia elimu wanayopata kuwa mabalozi watakaosaidia katika kuzuia uharibufu wa mazingira na kuwahimiza jamii kujenga utamaduni wa kupanda miti mipya na kulinda iliyopo kwa ajili ya manufaa yao ya sasa na baadae.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati alipowaongoza wanavyuo kutoka Vyuo mbalimbali katika upandaji miti ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhakikisha kila mtu anashiriki katika zoezi hilo.

Alisema kuwa wasomi kama wanavyuo wakiwa mstari wa mbele katika utoaji wa elimu katika maeneo yao yanayowazunguka na sehemu za baadae watakazopangiwa kazi ipo nafasi ya kuzuia uharibifu wa mazingira ikiwemo mistu kuendelea kuharibiwa.

Mwanri alisema kuwa jamii inawategemea sana wasomi katika kutoa elimu katika hatua ya awali ya kuzuia uharibifu kabla ya masuala mengine kama matumizi ya nguvu za dola hayafanyika katika kuzuia uharibifu usiendelee.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kitendo cha wanachuo hao kuomba kuweka alama katika Mkoa wa Tabora kinapaswa kuwa mwanzo kwao katika katika kupeleka elimu hiyo katika maeneo mbalimbali ya jamii inayowazunguka ili wananchi wengi waweze kutambua umuhimu wa kutoharibu mazingira na vyanzo vya maji.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tabora Idd Moshi aliwataka Wanachuo kuunga mkono juhudi za Mkuu huyo wa Mkoa wa kutaka kuigeuza sehemu ya kijana kwa kupanda miti miti na kurudisha uoto wa asili.

Alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora anafanyakazi nzuri ya kuhakikisha anasimamia agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha mikoa yote hapa nchini inapanda miti mingi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Moshi alisema kuwa wanachuo na jamii kwa ujumla wanalojukumu la kuhakikisha kuwa wanaunga mkono viongozi kwa kupanda miti sio katika maeneo ya umma katika maeneo wanayoishi.

Alisema kuwa wao wakiwa vijana wa CCM mkoa wa Tabora wameshapanda miti katika Wilaya ya Igunga , Nzega, Sikonge na Urambo katika kuunga mkono juhudi za viongozi wa Mkoa na Kitaifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad