HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 23 January 2018

SAIDA KAROLI KUPAMBA TAMASHA LA 15 LA SAUTI ZA BUSARA 2018

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Msanii wa nyimbo za asili Saida Karoli anatarajia kutuimbuiza katika tamasha la busara 2018 linalotarajia kuanza Februari 8, 2018 Ngome Kongwe mjini Unguja, Zanzibar.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mohamed alisema tamasha linazingatia Zanzibar na Tanzania sehemu mbalimbali duniani kwa kuwa linavutia mapromota wa kimataifa na kutoa fursa adhimu kwa wanamuziki wa Afrika Mashariki kuupeleka duniani kote.

Bw. Yusuf alisema kuwa wanamshukuru Mungu kwakuweza kukutana na msanii Saida Karoli ambaye amekubali kushiriki tamasha la sauti za Busara 2018 kwa vile sasa ni miaka 13 tokea ameweza kushiriki tamasha hilo.

Alisisitiza kuwa, orodha ya mwaka 2018 ni bora kuwahi kutokea kwa miaka yote 15 ya uhai wa tamasha hilo. "Ndani ya majukwaa matatu kwa siku nne, tamasha litakuwa na naonyesho 46 yenye hadhi ya kimataifa ambayo kwa asilimia 100 yatapigwa mubashara.

"Tamasha litawaleta pamoja wanamuziki wadogo na wakubwa kutoka katika viunga vyetu na hata nje ya nchi, likibeba dhumuni moja, huku tukisimama pamoja kupitia kaulimbiu ya Kuunganishwa na Muziki," alisema Yusuf.

Msanii wa nyimbo za asili Saida Karoli (pichani) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ushiriki wake katika tamasha la busara 2018 ambapo yeye mwenyewe alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuweza kushiriki tokea mwaka 2005. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud, Balozi wa Uswizi nchini Tanzania, Mhe. Florence Tinguely Mattli.
Waandishi wa Habari wakifuatilia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad