HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 23 January 2018

WAGOMBE 27 WATEULIWA MAJIMBO 2 KATA 4

Hussein Makame-NEC

WAGOMBEA 27 wa ubunge na udiwani wameteuliwa kugombea nafasi hizo katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Februari 17, mwaka huu katika majimbo mawili ya ubunge na kata nne.

Katika uteuzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki,  mgombea udiwani kupitita CCM katika kata ya Kimagai iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya  Mpwapwa mkoani Dodoma, amepita bila kupingwa.

Mbali na uteuzi huo, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika kata sita za Tanzania Bara wanatarajia kuteua wagombea wa udiwani wa kata hizo siku ya Jumatano ya tarehe 24 Januari, 2018 kukamilisha kata 10 zilizopangwa kushiriki Uchaguzi Mdogo wa Februari 17, 2018.

Akizungumzi uteuzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Hamis Mkunga amesema mgombea huyo wa CCMa amepita bila kupingwa baada ya mgombea wa CHADEMA kushindwa kurejesha fomu za uteuzi.

Amesema katika uteuzi wa wagombea Jimbo la Kinondoni, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo amewateua wagombea 12 ambao ni ambao ni Godfrey Maliza  kutoka chama cha TLP, Johnson Mwangosya  (SAU) na  Mwajuma Milambo kutoka UMD.
Mkunga amewataja wagombea wengine walioteuliwa kuwa ni John January Mboya  (Demokrasia Makini), Maulidi Mtulia (CCM), na Mary Mpangala wa DP.
Wengine ni Salim Mwalimu  (CHADEMA), Rajabu Salum (CUF), Mohamed Majaliwa (NRA), George Christian (CCK),  Ally Omari Abdallah (ADA THADEA) na Ashiri Kiwendu wa AFP 

Kuhusu uteuzi wa wagombea ubunge katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro, Mkunga amewataja wagombea wanne walioteuliwa kuwa ni Dk Godwin Mollel (CCM) Mdoe Azania Yambazi (SAU), Tumsifuheri Mwanry (CUF) naElvis Christopher MosiwaCHADEMA.

Katika kata tatu zilizobaki, Mkunga amevitaja vyama vya siasa vilivyopitisha wagombea ambao waliteuliwa katika kata ya Isamilo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza kuwa ni Chama cha CUF, DP, UDP, CCM, na CHADEMA.

Katika kata ya Manzase iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, wagombea walioteuliwa wametoka kwenye vyama vitatu vya CCM,CHADEMA na CHAUMA wakati wagombea watatu waliteuliwa kutoka vyama vya ACT-Wazalendo, CCM na CUF kugombea udiwani katika kata ya Madanga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Panganimkoa wa Tanga.

Kuhusu pingamizi kwa wagombea, Mkunga amesema hadi saa 10:00 jioni ya Januari 21, 2018, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi walipokea mapingamizi 10 kutoka Jimbo la Kinondoni mapingamizi manne na Kata ya Isamilo mapingamizi 6.

“Hakuna mapingamizi yaliyoripotiwa kutoka Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro na kata za Madanga na Manzase” amesema Mkunga na kuongeza:
“Mapingamizi ya Kinondoni, pingamizi moja limetolewa na CCM dhidi ya mgombea wa SAU, moja linatoka chama cha Dp kwa mgombea wake, lingine limewekwa na mgombea wa CUF na  wa CCM dhidi ya mgombea wa CHADEMA na la nne limewekwa na mgombea wa CHADEMA dhidi ya mgombea wa CCM”

Amefafanua kuwa katika kata ya Isamilo kulikuwa na mapingamizi sita mapingamizi manne ni ya mgombea wa CCM aliyewawekea pingamizi wagombea wa CHADEMA, CUF, DP na mgombea wa UDP.

Mapingamizi mengine ni kutoka kwa mgombea CHADEMA dhidi ya mgombea wa CCM na pingamizi lililowekwa na mgombea wa CUF dhidi ya mgombea wa CCM.

“Kinachofuata kwa sasa ni hawa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wanayapitia haya mapingamizi na kuyatolea maamuzi” ameeleza Mkunga na kufafanua kuwa:

Amesema kwa kuzingatia kifungu cha  44 (5) Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 na kifungu cha 40 (6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,wagombea waliokatiwa rufaa wana haki ya kukata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Kata sita zinazotarajia kufanya uteuzi tarehe 24 Januari, 2018 ni kata Buhangazaya Halmashauri ya Wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera, na kata ya Kanyeleleiliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza.

Nyigine ni  kata ya Mitunduruni yaHalmashauri ya Manispaa ya Singida mkoani Singida, kata za Kashashi, Gararagua na Donyomuruak zilizopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya  Siha  mkoa wa Kilimanjaro.

Kutokana na mgombea wa udiwani kata ya Kimagai kupitia CCM, kupita bila kupingwa, Mkunga amesema Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani unaofanyika Februari 17, 2018 utahusisha majimbo ya Siha na Kinondoni na kata tisa badala ya kata 10 za Tanzania Bara.

Katika uchaguzi huo jumla ya vituo 869 vya kupigia kura vitatumika na wapiga kura 349,211 wanatarajia kushiriki katika uchaguzi huo mdogo.

Mkunga amewaasa wagombea na vyama kuzingatie ratiba za kampeni kwa sababu kila chama na mgombea wake kimewasilisha ratiba yake ya kampeni lakini pia tufanye kampeni za kistaarabu kwani hilo ni suala la msingi sana.

Amevikumbusha vyama na wagombea kuheshimu maadili ya uchaguzi katika kipindi hiki cha kampeni kwani vyama vyote vimekubaliana kuheshimu maadili hayo na kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingisiku ya kupiga tarehe 17 Febraur mwaka 2018.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad