Serikali
imewataka watendaji
ngazi ya wilaya
na mkoa kusimamia kwa umakini zoezi la
upigaji chapa mifungo
linaloendea hapa nchini.
Agizo
hilo amelitoa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega wakati alipokuwa anazungumza na baadhi
ya watendaji wa mkoa wa Lindi kwenye
ziara yake ya kikazi ya siku mbili
mkoani humo.
Ulega alisema mtendaji yeyote
atakaye bainika kukwamishwa zoezi
hilo hata vumiliwa na kueleza kuwa kuna baadhi wanaonekana kukwamisha zoezi hilo kwa madai
ya kukosa bajeti ya kuendesha zoezi.
Wapo
watendaji wanaodharau zowezi hili kwa kweli serikali haita waacha salama alisema
Ulega.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi
amesema kuwa kunachangamoto kadha zilizosababisha baadahi
ya Halmshauri kushindwa
kutekeleza jukumu hilo
kwa wakati.
Zambi
alisema Halmshuari
ya wilaya Ruangwa ngo’mbe 268
kati 3000 wamepigwa chapa wakati wilaya ya Nachingwea ngombe
328 tayari wamekamilisha zoezi
hilo.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi ,Abdallah Ulega na akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Lindi mara baada ya kupokea ripoti ya ya mkoa huo.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi ,Abdallah Ulega akizindua zowezi la upigaji chapa mifugo katika mkoa wa Lindi.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Lindi.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi ,Abdallah Ulega
akizungumza na viongozi
mbalimbli,wafungaji juu ya kuhamasisha zowezi la ubikaji chapa mifugo
mkoa wa Lindi.
No comments:
Post a Comment