HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 3 January 2018

TRA INATARAJIA KUSAJILI WAFANYABIASHARA WADOGO MILIONI MOJA NCHI NZIMA

Na Chalila Kibuda, Globu
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imesema kuwa wanatarajia kusajili walipakodi wapya milioni moja (1,000,000)  ambao watalipa kodi ya shilingi Bilioni 1.5.

Kodi  zinazolipwa ndizo zinafanya serikali kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo  miundombinu ya barabara, afya, maji na huduma nyinginezo.

Akizungumza katika usajili wa kituo cha kusajili wafanyabiashara wadogo wadogo  cha Chanika, Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya amesema kuwa kampeni ya kusajili wafanyabiashara wa dogo ni endelevu.

Elijah amesema kuwa wananchi Wajitokeze kusajiliwa kadri kodi zinavyolipwa ndiyo zinafanya maendeleo ya nchi.

Amesema kuwa uhamasishaji wa ulipaji kodi na usajili utaendelea kwa kuweka vituo karibu na wafanyabiashara hao.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka hiyo, Richard Kayombo amewataka wananchi wa naoishi maeneo hayo kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kujiandikisha  na kusema kuwa zoezi hilo katika Kituo hicho Litadumu kwa muda wa juma moja.

Kayombo amesema wakitoka Manispaa ya Ilala watakwenda Manispaa ya  Temeke na baadaye  kufungua vituo katika maeneo mbalimbali" alisema Kayombo.

Aidha Kayombo amesema, Mamlaka hiyo imeamua kuja na kampeni hii  baada ya kutambua kuwa kulikuwa na usumbufu kwa Wafanyabiashara kupata TIN namba, kutokana na umbali kutoka wakazi wa eneo hilo hadi Vingunguti, na sasa wamesomea huduma hiyo na kwamba watakaojiandikisha hawana ulazima kulipa kodi siku hiyo hiyo.

Pamoja na hayo amewatahadhalisha wananchi kutolaghaiwa na matapeli kwani kazi hiyo inafanywa na TRA yenyewe na hakuna wakala aliye pewa kazi hiyo.
  Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya akizungumza na waandishi habari juu ya usajili wa wafanyabiashara wadogo katika kituo cha Chanika jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Regina Urio (kulia)  akimhudumia mfanyabiashara (kushoto) aliyefika katika kituo maalum kilichoteuliwa na mamlaka hiyo kilichopo Chanika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusajili na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad