HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 4, 2018

TATIZO LA MAJI MKURANGA KUWA HISTORIA- NAIBU WAZIRI ULEGA

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi  wa Kijiji cha  Mwanambaya wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani wakati wa ziara yake ndani ya Jimbo la Mkuranga.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema suala la maji Mkuranga ni tatizo la muda lakini sasa matumaini yameanza kuonekana baada ya  benki ya Dunia kuleta  mradi wa maji wa visima 29 utakaokuwa na thamani ya zaidi ya bilioni mbili.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwanambaya, amesema kuwa mradi wa maji utakuwa historia kutokana na hatua zinazochukuliwa na serikali. Amesema katika ziara zake amekuwa akikutana na changamoto za maji lakini hatua zimeanza kuchukuliwa kwa kiangazi cha mwaka huu maji yatakuwa tayari.

Katika Mkutano huyo amehidi kutoa bati 100 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili ya shule ya Msingi Mwanambaya.

Naibu Waziri huyo ameiomba kamati ya kijiji kukutana na mganga Mkuu ili waweze kuipandisha dispensari hiyo kwenda kituo cha afya.

Mbali na hilo wananchi wa kijiji cha Mwanambaya  wamemuomba mbunge Ulega kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kulipwa stahiki zao za kupitiwa  na mradi wa mabomba ya gesi ya  Kilwa Energy.
Sehemu ya wananchi wa mwanambaya katika Mkutano. picha ,Emmanuel Massaka,Globu ya jamii


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad