HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 11, 2018

SUMATRA PWANI YAKEMEA KUPANDISHWA NAULI KIHOLELA KWA MABUS YAENDAYO MIKOANI

 Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

OFISA mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) Mkoani Pwani, Omary Ayoub amekemea tabia ya kupandishwa kwa nauli inayofanywa na baaadhi ya mabasi ya abiria yaendayo mikoani. Aidha mamlaka hiyo, imetoa wito kwa abiria kufunga mkanda pasipo kudharau kwa ajili ya usalama wao.

Ayoub aliyasema hayo, wakati wa ukaguzi wa magari ya abiria yaendayo mikoani  katika stand kuu ya Mailmoja, Kibaha, ukaguzi ambao unafanyika kwa ushirikiano kati ya Sumatra na kamati ya usalama barabarani mkoani humo. Alisema changamoto kubwa waliyonayo katika mkoa huo ni baadhi ya abiria waendao mikoani kuzidishiwa nauli tofauti na nauli halali.

Ayoub, alielezea wamepokea taarifa kutoka kwa abiria hao kuwa kuna wahusika wa mabasi ambayo yamekuwa yakipandisha nauli huku kwenye tiketi zao wakiwa wanaandikiwa nauli halali jambo ambalo linawakandamiza abiria. Alisema hawatamvumilia dereva ,kondakta wala mmiliki yoyote anayehusika kukiuka taratibu za usafirishaji. Ayoub alieleza,wanapobaini kuwa madereva au wamiliki wamekiuka taratibu zilizopo kisheria huwachukulia hatua mbalimbali ikiwemo kuwatoza faini ama kuwashtaki mahakamani.
Aliwaomba wananchi na abiria kutoa taarifa juu ya ukiukwaji wa taratibu za usafirishaji kwa wale wanaopandisha nauli na kuandika nauli zisizo sahihi kwenye tiketi zao.

“Tunaomba ushirikiano juu ya suala hili ,tunafuatilia na kusimamia ili kuwasaidia wananchi ambao hawajui haki zako na wapi waende kufikisha kero hizo"

"Msiogope kusema na kuwataja hawa wanaopandisha nauli ,;:Msilipe nauli zaidi ya iliyoandikwa kwenye tiketi " alisema Ayoub.

Akizungumzia umuhimu wa kufunga mkanda wakati wa safari ,Ayoub alisema abiria wanaona hakuna umuhimu wa kufunga mikanda lakini waelewe ni muhimu kwao. Alisema kufunga mikanda ipo kisheria ya mwaka 2007 ya Sumatra inayotakiwa abiria wafunge mikanda kwa usalama wao.

"Inastaajabisha unakuta abiria wanafunga mkanda wakiona askari wa usalama barabarani ama Sumatra wakikagua magari hayo " alisema Ayoub.

Kwa upande wake ,mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoani Pwani ,Josephine Protas aliwataka madereva na wamiliki kufuata sheria na taratibu. Aliwaasa pia madereva kuacha kuendesha kwa mwendo kasi na kutumia vileo wakati wakiendesha. Josephine alisema ,kuendesha pasipo kuwa makini na tahadhari ukiwa barabarani kunasabababisha ajali zembe na kuhatarisha maisha ya watu wasio na hatia. Aliyataka magari madogo ya abiria yanayofanya safari zake Mbezi-Mlandizi-Chalinze kutoa tiketi kwa abiria ili kuondoa usumbufu kwa abiria 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad