HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 11, 2018

WANANCHI WASHAURIWA KUTOISUBIRI SERIKALI KUWAFANYIA KILA KITU

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akitengeneza tofali kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Kata ya Kakese iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi katika ziara yake ya siku mbili kuamsha ari ya wananchi katika kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amewashauri wananchi wa Kata ya Kakese Wilayani Mpanda Mkoani Katavi kutoisubiri Serikali kuwafanyia kila kitu wakati wanana uwezo wa kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili katika maeneo yao. Ameyasema hayo wakati wa ziara yake mkoani Katavi yenye lengo la kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Ameongeza kuwa lengo la ziara hiyo ni kufuatilia namna ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii ambayo inasisitiza ushirikishwaji wa jamii katika maamuzi, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli au miradi ya maendeleo ikiwemo upanuzi na uendelezaji wa miundo mbinu mijini na vijijini kama Shule, Barabara, Zahanati na Maghala kwa kutumia rasilimali zilizopo.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga akitengeneza tofali kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Kata ya Kakese iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi katika ziara ya siku mbili ya Naibu Wazriri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kuamsha ari ya wananchi katika kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Wizara yake imeamua kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi za Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushiriki kwa vitendo kwa kufanya kazi na jamii kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu  ya Elimu, Afya, Kilimo, Barabara na Viwanda.

“Hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii inayotoa matokeo yenye mashiko na tija katika jamii. Tumieni stadi na mbinu shirikishi kuwezesha maendeleo jumuishi ambapo makundi yote katika jamii yanashiriki katika maendeleo yao alisistiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile ameeleza  kuwa pamoja na msisitizo uliotolewa na Sera kuwa wananchi ni kitovu cha maendeleo, taarifa kutoka kwa wadau mbali mbali wanaofanya kazi na jamii zinaonesha kuwa ari ya wananchi kushiriki katika kazi za maendeleo imeshuka kwa kiasi kikubwa ila kwa sasa wamejipanga kuirudisha ari ya wananchi kujitolea.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kulia) akikabidhi moja ya mifuko 42 ya saruji kwa uongozi wa Kata ya Kakese Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi katika kuunga mkono juhudi za wananchi katika kujiletea maendeleo yao.

“Hali hii ya wananchi kutojitolea na kushiriki katika shughuli za maendeleo inapelekea kutokamilika na kukosekana kwa uendelevu wa miradi mingi ya maendeleo ambayo inahitaji nguvu ya wananchi alisema Mhe. Dkt Ndugulile

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga amempongeza  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kwa kuamua kushirikiana na wananchi na viongozi kufanya kazi katika kuamsha ari ya wananchi kujitolea katika shughuli za maendeleo katika kujenga shule ya Sekondari ambayo itasaidia watoto kupata elimu jirani na makazi yao.

Mmoja ya wananchi wa Kata ya Kakese Bw. Fedrick Kanangu ameishukuru Serikali kwa kuunga mkono jitihada zao na kuwashauri wananchi wenzake kuendelea kujitolea katika kufanya kazi za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akizungumza na wananchi wa Kata ya Kakese Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi na kuwashauri kutoisubiri Serikali kuwafanyia kila kitu hata yale ambayo wanaweza kuyafanya kwa nguvu zao katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi katika kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

“Ushiriki wa jamii katika kutekeleza kazi na miradi ya maendeleo huharakisha kufikiwa kwa malengo mbalimbali ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla” alisema Bw. Kanangu.

Wote kwa pamoja tuendelee kushirikiana na kusukuma gurudumu la maendeleo mbele kwa kuweka uzalendo mbele na kuchapa kazi kwa bidii na kwa kuwaunga mkono kwa kazi za maendeleo wanazofanya wananchi wa Kata ya Kakese Naibu Waziriwa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alichangia  mifuko 42 ya saruji.
Baaadhi ya wananchi wa Kata ya kaseke wakimsikiliza Naibu Wazriri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile mara baada ya kushirikiana naye kufyatua tofali kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kakese iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi. Picha Zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad