HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 9 January 2018

RAIS MAGUFULI AMEMSIFU LOWASSA KWA KUFANYA SIASA ZA KISTAARABU

*Asema ni mwanasiasa wa tofauti na wengine
*Amuahidi kumpa ushirikiano,apokea ushauri wake

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli amemuelezea Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kuwa ni mwanasiasa mstaarabu na kuahidi kumpa ushirikiano.

Ameongeza hata wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, Lowassa hakuna mahali popote ambapo amemtukana na kutumia nafasi hiyo kusema mzee huyo ni tofauti na wanasiasa wengine nchini.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu mstaafu Lowassa ambapo wamezungumza mambo mengi. Akimuelezea Lowassa, Rais, Magufuli amesema ni mzee huyo ni moja kati ya wanasiasa ambao wamekuwa wakifanya siasa za kistaarabu tofauti na wengine.

" Wakati wa uchaguzi mkuu hakuna mahali popote akiwa kwenye kampeni mzee Lowassa amenitukana au kutukana mtu yoyote.

"Kikubwa niseme tu nampongeza .Labda wale wapambe wake ndio walikuwa wanatukana na naamini hakuwatuma. Etii mzee Lowassa uliwatuma? Lowassa akajibu "hapana sijawatuma".

Rais Magufuli akafafanua kuwa "Wapambe ndio walikuwa wanaropoka na kufanya mambo mengi lakini kwa mzee Lowassa amekuwa akifanya siasa za kistaarabu."

Hivyo ndio maana anampongeza na kumtakia maisha mema na yeye Rais akiwa kiongozi wake ataendelea kutoa ushirikiano kwake. Amesema akiwa na mzee Lowassa wamezungumza na kushauriana mambo mengi ambayo hawezi kuyasema.

"Tutaendelea kushirikiana na naamini ataendelea kunishauri kwa maslahi ya nchi yetu,"amesema.

Amumelezea Lowassa kuwa amefanya mambo mengi mazuri kwa nyakati tofauti na aliyoyafanya lazima mchango wake utambulike. "Namshukuru na kumtakia heri ya mwaka mpya".

LOWASSA AIONA TANZANIA YA MATUMAINI

Kwa upande wake Lowassa pamoja na mambo mengi ameelezea namna anavyoiona Tanzania ya miaka mitano ijayo.

"Naiona Tanzania yenye matumaini mapya kwa Watanzania,"amesema Lowassa wakati anajibu swali ambalo ameulizwa anaionaje Tanzania ya miaka mitano ijayo?

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad