HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 9 January 2018

KLABU SIMBA SPORT YAREJEA LEO JIJINI DAR ES SALAAM


 Wachezaji wa Simba SC, Nicolaus Gyan na Asante Kwasi wakiwasili leo jijini Dar es Salaam kutokea visiwani Zanzibar  mara baada ya kuondolewa katika Michuano ya  Kombe la Mapinduzi baada ya kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi A.
 Mshambuliaji wa Wekundu wa Msimbazi,  Shiza Ramadhani Kichuya akikataa kuzungumza na waandishi wa habari bandarini hapo mara baada ya kuwasili leo Jijini Dar es salaam akitokea visiwani Zanzibar  mara baada ya kuondolewa katika Michuano ya  Kombe la Mapinduzi .
 Baadhi ya washabiki wa Simba SC wakishangilia mara baada ya timu hiyo ilipokuwa ikirejea nyumbani mara baada ya kuondolewa katika Michuano ya  Kombe la Mapinduzi.
Mshabiki wa Simba SC, Willium Mazoba akizungumza na Michuzi Blog amesema kuwa amesikitishwa kwa timu yake kupoteza michuano hiyo na kuwataka walimu kujipanga kwa ajili ya ligi kuu Tanzania Bara. (Picha na Agness Francis wa Blogu ya Jamii)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad