HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 11 January 2018

RAIS DKT. MAGUFULI, LOWASSA WAMETOA FUNZO KWA VIJANA-RC GAMBO

Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii.

MKUU wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa kitendo cha Rais, Dkt. John Magufuli kufanya mazungumzo na waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kumetoa funzo kwa vijana. 

Gambo ametoa kauli hiyo wakati anazungumza na Michuzi Blogu, jijini Dar es  Salaam ambapo amesema kitendo cha Lowassa kuomba kwenda kuonana na Rais Ikulu na kukubaliwa kuna funzo kubwa ndani yake na hasa vijana kutambua siasa si uadui. 

Amesema Rais, Dkt.Magufuli amethibitisha kuwa yupo kwa ajili ya watanzania wote bila kujali dini, kabila au itikadi za kidini na kubwa zaidi ameonesha mamba ambavyo ni msikivu kwa anaowaongoza. 

Amesema hata Lowassa wakati anazungumza akiwa Ikulu amesema amefarijika kukutana na Rais Magufuli na kufanya mazungumzo. 

"Kuna some kubwa la kujifunza hasa kwetu vijana kutambua siasa si uadui. Na unapokuwa kiongozi unastahili kumsikiliza kila mtu.Kwangu naona kuna kitu ambacho Kama kijana lazima tujifunze kutoka kwa Rais wetu,"amesema. 

Kuhusu wanaomshambulia Lowassa kwa uamuzi wake wa kwenda Ikulu amesema hao ni wachanga wa siasa.

"Nimemsikiliza Mwenyekiti wa  Chadema Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema lakini nachokiona kutoka kwako wanasumbuliwa na uchanga wa siasa tu,amesema Gambo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad