HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 27, 2018

Kamishna Mkuu mstaafu Mwasalla atoa msaada wa sare Girl Guides

 Kamishna Mkuu wa zamani wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Faithjoy Mwasalla (kushoto), akikabidhi msaada wa sare na fulana kwa chama hicho katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya chama hicho, Dar es Salaam. Kutoka kulia ni; Girl Guides Asha Ramadhan, Rhoda Idd, Mariam Nuru, Salma China, Kiongozi wa Girl Guides, Rehema Kijazi, Kiongoizi wa Girl Guides Temeke, Leonida Komba na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Girl Guides wakimshukuru Mwasalla kwa kuwapatia msaada huo.
 Mwasalla akipongezwa na Kiongozi wa Girl Guides Temeke, Leonida Komba.

 Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba akizungumza na Guides wakati wa hafla hiyo
 Mwasalla akionesha moja ya sare hizo 
 Girl Guides wakibeba msaada huo
Girl Guides wakiwa wamevaa baadhi ya sare walizopewa msaada.


Na Richard Mwaikenda, Msasani.


Kamishna Mkuu wa zamani wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Faithjoy Mwasalla ametoa msaada wa sare na fulana kwa chama hicho.


Hafla hiyo ilifanyika leo katika Makao Makuu ya TGGA, Msasani Dar es Salaam, mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Grace Shaba na maofisa wengine.


Msaada huo aliukabidhi kwa Girl Guides kutoka shule za Wilaya ya Temeke, walioongozwa na Kiongozi wa TGGA wa wilaya hiyo, Leonida Komba.


"Sisi Tgga tunaamini katika kujitolea hivyo nikiona wenzangu wanastawi nafurahi sana, ndiyo maana nimetoa msaada huu ili Girl Guides wapendeze na waendelee vizuri wawe viongozi wazuri wa kesho, kwani anayekulia malezi ya girl Guides anakuwa na maisha mazuri yenye nidhamu." Amesema Mwasalla huku akipigiwa makofi.


Pia Girl Guides waliopokea msaada huo kwa niaba ya wenzao, walishukuru sana kupata msaada huo na kwamba wamejifunza suala la kujitolea pamoja na mshikamano na umoja uliomo ndani ya chama chao na kuahidi kuendeleza mambo hayo muhimu.

Kiongozi wa Girl Guides Wilaya ya Temeke, Leonida Komba naye kwa niaba ya viongozi wa TGGA Manispaa ya wilaya hiyo alitoa shukrani kwa Mwasalla ambaye ni mmoja wa waasisi wa chama hicho, kwa kutoa msaada huo na kumtakia aendelee na moyo huo wa kizalendo ambao ni watu wachache wanao, aliomba Mungu amjalie na ambariki sana.



Naye Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba, alimshukuru Mwasalla kwa Moyo aliouonesha wa kujitolea kwa kutoa msaada huo hasa katika kipindi hiki kigumu ambacho vijana wengi hawana uwezo wa kununua sare,na kwamba msaada huu ameutoa wakati muafaka. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad