HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 27, 2018

NAIBU WAZIRI AKUKAGUA MAKAZI YA ASKARI NA MAENEO YA POLISI WALIYOUZIWA WANANCHI KINYUME NA UTARATIBU

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuuliza maswali Mhandisi wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Pascal MacORWA (kushoto), alipotembelea eneo la Tunguu lililovamiwa na wananchi, ambalo mmiliki halali ni jeshi la Polisi. Wakwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja,Makarani Khamis na watatu kulia ni Mkuu wa mkoa huo, Hassan Khatib Hassan.Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Makarani Khamis , akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, juu ya eneo la Tunguu lililoko Mkoa wa Kusini Unguja ambalo ni mali ya Jeshi la Polisi, hivi sasa likimilikiwa na wananchi kinyume cha sheria.Kushoto ni Mkuu wa mkoa huo, Hassan Khatib Hassan. Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyeshwa na Mhandisi wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Pascal MacORWA, ramani ya moja ya maeneo yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa ziara ya naibu waziri kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi mkoani hapo.Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo,Hassan Khatib Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan, akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua makazi ya askari polisi yanayoonekana pichani, yaliyopo eneo la Machui, lililopo Mkoa wa Kusini Unguja.Naibu Waziri yupo Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi na makazi ya askari.Kulia ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan, akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kukagua eneo yalipojengwa maduka ya biashara ambayo wamiliki wamenunua viwanja hivyo vya Jeshi la Polisi kinyume na utaratibu. Naibu Waziri yuko Visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Mkoa Kusini Unguja alipowasili leo mkoani hapo kwa ziara ya kikazi ya kukagua maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya polisi na makazi ya askari.Kulia ni Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani hapo.


IMENDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad