HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 25, 2018

ERIKALI YASITISHA SHUGHULI ZA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA WALIOKIUKA SHERIA.

Na:Mwandishi wetu.
Serikali yasitisha Shughuli za Kampuni Tatu (3) za Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira hapa Nchini kutokana na kukiuka matakwa ya sheria ya Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999 na Kanuni zake.

Akitoa tamko la Serikali kuhusu Kusitishwa kwa Shughuli za Kampuni hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi na wadau mbalimbali kuhusu utaratibu unaotumiwa na baadhi ya Wakala Binafsi wa huduma za Ajira nchini.

Kampuni zilizofutiwa usajili baada ya kukiuka sheria ni pamoja na  Sasy Solution Company Ltd, Bravo Job Centre Agency na Competitive Manpower International Ltd ambapo Kampuni hizo haziruhusiwi kujihusisha na shughuli za Uwakala  Binafsi wa Ajira  nchini.

Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa uchunguzi umebaini  ukiukwaji wa taratibu za usajili ambapo baadhi ya Mawakala wamekuwa wakitumia nyaraka zilizopatikana kwa njia isivyo halali katika kujipatia leseni za uwakala hali iliyowawezesha kukwepa kodi na kujipatia faida.

Aliongeza kuwa ukiukwaji wa taratibu za kisheria umeleta athari mbalimbali kwa wafanyakazi hasa kwa wale wanaoenda kufanya kazi Mataifa ya Nje ambapo wafanyakazi hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji katika ajira, malipo ya mishahara na stahiki mbalimbali.

Aidha, Mhe. Mhagama amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imesitisha mara moja shughuli za Mawakala Binafsi wa huduma za Ajira zinazohusika na kuwatafutia kazi wafanyakazi nje ya nchi (cross border placement) hadi hapo Serikali itakapoleta mfumo wa kusimamia jambo hili na kutoa taarifa kwa umma.

Vile Vile, Waziri Mhagama amemwagiza Kamishna wa Kazi kuhakikisha kuwa ndani ya wiki mbili kuzifanyia uhakiki Wakala zote zilizosajiliwa kuona kama wametimiza na kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia Wakala Binafsi za Ajira, Pia aliiasa Timu ya wakaguzi itakayoundwa na Wizara ikikiuka miiko ya ukaguzi na kuficha udhaifu wa mawakala hao hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa Mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akitoa tamko la Serikali leo mjini Dodoma kuhusu Kusitishwa kwa Shughuli za Kampuni zinazotoa huduma ya Uwakala Binafsi wa Ajira baada ya kukiuka sheria ni pamoja na Sasy Solution Company Ltd, Bravo Job Centre Agency na Competitive Manpower International Ltd ambapo Kampuni hizo haziruhusiwi kujihusisha na shughuli za Uwakala  Binafsi wa Ajira  nchini, Januari 25, 2018.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama leo mjini Dodoma wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu Kusitishwa kwa Shughuli za Kampuni zinazotoa huduma ya uwakala binafsi wa Ajira baada ya kukiuka sheria Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999 na Kanuni zake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad