HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 31, 2018

WABUNIFU WA MITINDO WAZINDUA CHAMA CHAO

Na Karama Kenyenko, Globu ya jamii
WABUNIFU wa mitindo nchini wamezindua chama chao kitakachojulikana Chama cha Mitindo Tanzania(FAT) ambacho kitakuwa na jukumu la kusimamia na kuendeleza maslahi ya sekta hiyo.

Uzinduzi huo wa FAT umefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuelezwa hatua hiyo imekuja baada ya kupokea ujumbe kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia kwa Mkurugenzi wa Kukuza Sanaa na Masoko kuwataka wabunifu wawe na chama chao kitakachokuwa kinajihusisha na masuala ya utindo.

Mwanzilishi wa Chama cha Mitindo Tanzania Mustafa Hassanali amesema FAT kimeundwa ili kuongeza nguvu na taaluma ya uwezo wa kukuza na kuimarisha sekta ya mitindo nchini.

"Sekta ya mitindo Tanzania inakuwa kwa haraka sana, wadau wake wanakumbana na changamoto nyingi lakini bado tuna uhakika wakati wa mafanikio kupitia kuanzishwa kwa chama hiki ikiwemo kuunga juhudi za Rais, Dk. John Magufuli ya kuifanya nchi yetu kuwa katika uchumi wa viwanda wa kati ifikapo mwaka 2025,"amesema.

Kwa upande wake Mama wa Mitindo na Mwanzilishi wa Lady In Red nchini  Asia Idarous amesema chama hicho hakijaundwa kwa ajili ya wabunifu tu bali hata kwa wadau wote wa sekta ya mitindo,majukwaa mbalimbali ya mitindo, taasisi za mitindo, wanamitindo(models) na wanamitindo wanaopanga mavazi (Stylish).

Mbali na hao wengine ni wapiga picha wa mitindo,makampuni ya nguo, wazalishaji na wauzaji wa mavazi mbalimbali.


"Nimetembea katika majukwaa mengi ya mitindo duniani na nchi mbalimbali lakini nchi zenye maendeleo makubwa katika sekta ya mitindo ni zile zilizofanya juhudi ya kuunda chama kitakachosimamia maslahi yao ila bado hatujachelewa kufanya hivyo," amesema Asia Idarous.
 Mwañzilishi wa Chama cha wanamitindo (FAT), Mustapha Hassanali, akizungumza na waandishi wa Habari juu ya kuanzishwa kwa chama cha wanamitindo nchini.
  Katibu Mtendaji toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Chama  cha Wanamitindo Tanzania (FAT) mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania Adrian Nyangamalle na kushoto ni Mwanamitindo mkongwe nchini Bi. Asia Idarous
Katibu mtendaji Baraza la Sanaa la Taiga, Godfrey Mngereza, mwenye shati la kitenge, akizindua chama cha wanamitindo Tanzania ( FAT), jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad