HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 11 January 2018

ATCL YAKUMBUKA WATOTO YATIMA

Na Said Mwishehe,  Globu ya jamii
SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) limetoa msaada wa vyakula , mafuta , sabuni, nguo,sukari na madaftari kwa Kituo cha Mwandaliwa ambacho kinaelea watoto yatima.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa ATCL, Christina Tungaraza amesema thamani ya msaada huo umegharimu sh.milioni tano ikiwa ni kutambua umuhimu wa jamii kusaidia wasiojiweza na hasa watoto yatima.

"Tumeanza mwaka mpya kwa kusaidia watoto walioko kwenye kituo hiki na mbali ya kuleta msaada huu, tunataka kuzungumza na uongozi kuona ni maeneo gani tunaweza kuendelea kusaidia" amesema Tungaraza.

Amefafanua msaada ambao wameutoa kwa watoto hao ni ule ambao unatumika na kwisha na sasa wanachotaka ni kutoa msaada ambao utadumu zaidi.

Tungaraza amesema shirika lolote la biashara mteja lazima awe namba moja kwao na wanatoa kipaumbele kwa mteja na kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi.

Akiuzungumzia msaada huo Mwanzilishi na Mkurugenzi wa kituo hicho, Halima Mpeta ametoa shukrani kwa msaada huo wa ATCL na kuiomba jamii kuiga mfano huo kwa kusaidia watoto walioko hapo.

Amesema kuna vitu ambavyo si lazima kuvifanya lakini la kusaidia watoto yatima lina umuhimu wake na ndio maana tunaomba wenye uwezo wasaidie.

"Tunawashukuru ATCL kwa msaada wao, tunauthamini sana na tunathamini wafanyakazi wote na walichotoa Mungu atakirejesha na kulifanya shirika hilo kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha,"amesema Mpeta.
Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Bi. Christina Tungaraza akikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa Bi. Halima Ramadhani Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es salaam wakati wafanyakazi wa shirika hilo walipotembelea na kuwafariji watoto Yatima katika kituo hicho leo, Msaada uliotolewa una thamani ya shilingi milioni tano
Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Bi. Christina Tungaraza akishiriki kuimba wimbo na watoto wa kituo hicho pamoja na wafanyakazi wenzake.
Wafanyakazi wa ATCL wakicheza pamoja na watoto wa kituo hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad