HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 24, 2017

WAVAMIZI WA HIFADHI YA MISITU WILAYANI YA GAIRO WAONDOLEWA

 Mkuu wa Wilaya Mhe. Siriel Shaidi Mchembe (kushoto) akiwa pamoja na Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Bw. David Mahiba pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wakati wakitoa elimu kwa wananchi walioshiriki zoezi hilo kwa asilimia 100 kwa amani na upendo.

Wananchi wakifuatilia mkutano huo.

Na Mwandishi Wetu.

Wadau wa mazingira nchini Tanzania wameombwa kujitokeza kuinusuru wilaya ya Gairo ambayo inahekari zaidi ya 3,000 zilizokuwa zimevamiwa waharibifu wa mazingira.

Kauli hiyo imekuja hivi karibuni baada ya Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa lakuwaondoa wavamizi wa Misitu ya Hifadhi kabla ya Disemba 31, 2017.

Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo alipokuwa akiahitisha Bunge la mjini Dodoma Novemba 18, 2017.
Kati ya maeneo ambayo yalikuwa na uvamizi na uharibifu mkubwa wa mazingira ni Misitu ya Hifadhi Wilaya ya Gairo.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya walifanya vikao na wananchi huku wakipitia muhtasari ya vikao vya nyuma vya ushirikishwaji kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya hadi Mkoa vya kuwaondoa wavamizi hao.
Vibanda vya wavamizi wa Hifadhi ya Misitu Gairo vikiteketezwa kwa moto.
Miti ya asili yenye zaidi ya miaka 35 ikiteketezwa kwa ajili ya kutengeneza mkaa. Sehemu kubwa ya miti hii ni miti ya mbao ngumu aina ya mitondoro.
---
Aidha kupitia taarifa ya mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji hicho ambayo ilisomwa na mwenyekiti wa Kijiji ikibainisha utengwaji wa maeneo mbalimbali zikiwemo ekari 1,000 za hifadhi walizogawiwa wananchi kwa ajili ya kilimo.

Vikao vilifanyika kuanzia mwaka 2012 wakati huo Mkuu wa Mkoa akiwa Mhe. Kanali Machibya. Baadae Mkuu wa Mkoa alikuwa marehemu Joel Bendera ambapo nyumba kadhaa ziliteketezwa.
Licha ya juhudi zote hizo bado wavamizi hao waligoma kutoka.

Hivyo basi, kwa kauli ya Waziri Mkuu zoezi limefanikiwa wavamizi wote wameondoka katika Misitu Hifadhi ya No. 30 Kijiji cha Kumbulu Kata ya Chanjale na nyumba zote ziliteketezwa kwa moto.

Eneo hilo la misitu lina ukubwa wa ekari 3,000 limepakana na Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa na kutokana na uharibifu huo mkubwa umesababisha hali kubwa ya ujangwa kwa Gairo na maeneo ya Dodoma.

Ikumbukwe kuwa Wilaya ya Gairo inategemeana sana na Mkoa wa Dodoma kwenye hali ya hewa kwani uwanda wa juu wa Gairo kupitia milima iliyopo Tarafa ya Nongwe ni kichocheo kikubwa cha hali ya hewa nzuri makao makuu ya nchi Dodoma. Ipo misitu mingine kama misitu ya Hifadhi ya Ukaguru ambayo ni namba tano kwa ukubwa nchini Tanzania. Ipo misitu mingine mikubwa mitatu.

Zoezi  hilo liliweza kukamilika kwa asilimia 100 lkinachofuata ni operesheni kubwa ya kupanda miti inayofanywa Wilayani kwa usimamizi makini wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia Meneja wake, Bw. David Mahiba. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad