HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 24 December 2017

NAIBU WAZIRI SHONZA AFUNGA TAMASHA LA MICHEZO KARATU

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana Shonza (Wa pili kushoto) akipiga risasi hewani kuashiria kuanza kwa mbio za Kilomita kumi wakati wa kufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika mjini Karatu tarehe 23/12/2017, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe Teresia Mahongo.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana Shonza akishiriki mbio za Kilomita tano wakati wa kufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika mjini Karatu tarehe 23/12/2017. Kutoka Kulia wakwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi. Teresia Mahongo, Afisa Utamaduni na Michezo Ndg.Laurent P. Manonga na wakwanza kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Karatu Ndg. Waziri Mourice.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mhe Juliana Shonza (Wa mbele katikati) akimaliza mbio za Kilomita tano aliposhiriki kufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika mjini Karatu tarehe 23/12/2017.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza akimkabidhi  zawadi ya fedha taslimu shilingi laki tano mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita kumi Ndg Emmanuel Giniki wakati wakufunga Tamasha la Michezo Karatu lililofanyika mjini Karatu tarehe 23/12/2017.
 Washiriki wa mbio za kilomita kumi wakijiandaa kutimua vumbi wakati wakufunga Tamasha la Michezo Karatu  lililofanyika mjini Karatu tarehe 23/12/2017.
Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania na Mratibu Mkuu wa Tamasha la Michezo Karatu Ndg. Filbert Bayi akizungumza wakati wa kufunga Tamasha  hilo lililofanyika mjini Karatu tarehe 23/12/2017. Waliokaa wakwanza kulia ni Ndg. Waziri Mourice Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Karatu, wapili ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi Teresia Mahongo na  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad