HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 15, 2017

SERIKALI YATAMBUA MCHANGO WA TIA KUANDAA WATAALAM WA UHASIBU

Ofisa Mtendaji Mkuu Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA), Dk. Joseph Kihanda akizungumza na wahitimu pamoja na wageni wakati wa mahafali ya 15 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) yaliyofanyika chuoni hapo leo jijini Dar es Salaam.

Said Mwishehe, Blogu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Ashatu Kijaji amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na taasisi katika kuandaa wataalam wa tasnia ya uhasibu , biashara ,masoko na rasilimali watu.

Dk.Kijaji amesema hayo leo kwenye mahafali ya 15 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA), Dar es Salaam.Jumla ya wahitimu 3,538 wametunikiwa vyeti kwa ngazi mbalimbali za kitaaluma.

"Endeleeni kutekeleza majukumu yenu kwa weledi, na sisi Serikali tutaendelea kuwaunga mkono.Idadi kubwa ya wahitimu waliopo mbele yetu ni ushahidi tosha wa juhudi na ushirikiano mzuri baina ya Taasisi na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango,"amesema.

Kuhusu mahafali hayo, amesema amepata fursa kujua baadhi ya mafanikio,changamoto na matarajio ya TIA kupitia hotuba iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wake Dk.Joseph Kihanda.

Amesema rasilimali zilizopo ni ndogo na vipaumbele ni vingi.Ili kutatua changamoto za taasisi hiyo ni muhimu kubuni mbinu mpya za kuimarisha mapambano kupata mafanikio makubwa zaidi.

Pia amesema azma ya kuanzisha kozi ya Shahada ya pili nayo ni nzuri ili kuongeza nafasi ya kutoa mchango wao kwenye Taifa, na kuwa na mapato ya uhakika.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Wakili Said Chiguma amesema Taasisi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa na kuwezesha kutoa wahitimu wa sifa za kutukuka , kwa ushindi mkubwa kitaaluma na ufanyakazi wa utofauti sehemu mbalimbali kazini.

"Kwa miaka miwili mfululizo 2015/2016 na 2016/2017 imeongoza kutoa wafaulu wengi wa Shahada ya juu kitaaluma ya uhasibu na ile ya taaluma ya ugavi,"amesema.

Ameongeza pamoja na mafanikio ya kitaaluma na mipango ya kubadilisha mitaala kulingana na soko la ajira,Taasisi inachangamoto mbili kuu.Moja uhaba wa wahadhiri kulingana na idadi ya wanafunzi na upungufu wa miundombinu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad