HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 15, 2017

MAHAFALI YA 15 YA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII YAFANA LEO JIJINI DAR.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewataka wananchi kushirikiana na serikali katika kuvitangaza vivutio vya utalii ili kuongeza pato la taifa.

Amezungumza hayo  leo wakati wa mahafali ya 15 ya Chuo cha Taifa cha  Utalii yaliyofanyika kwa kuunganisha matawi ya chuo hicho nchini.

Hasunga amewatunikia wanafunzi 129 wakiweza kutunukiwa shahada na astashahada katika fani za upishi, usafi wa vyumba, uhudumu wa chakula na usafirishaji wa watalii.

Katika mahafali hayo, Niabu Waziri Hasunga amewataka wananchi smabamba na wadau mbalimbali wa utalii kushirikiana na serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii  kuutangaza utalii kwani ni sekta mtambuka.

Kwa sasa seriikali mfumo wa kuwasajili wanafunzi wote walisomea masuala ya utalii ili kuweza kufahamu idadi yao ukamili na pia kuweza kuwafahamu wale ambao wapo katika sekta ya utalii wakiwa hawajapitia katika mafunzo yoyote.
Bendi ya jeshi ikiongoza maadamano ya mahafali ya kumi na tano(15) ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katika)  akiwa kwenye maandamano kwa ajili ya mahafali ya kumi na tano ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini ambapo  wahitimu 129 wa stashahada na astashahada wametunukiwa vyeti vyao  jijni Dar es Salaam.  Kulia mbele ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii. Dkt. Shogo Muzola na kulia na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo hicho, Bernadetha Ndunguru.
 Baadhi ya wahitimu wa stashahada na astashahada wakiwa kwenye maandamano wakati wa ya mahafali ya kumi na tano ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini 

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akifungua pamoja na kuzungumza na wahitimu na wageni waalikwa wakati  mahafali ya kumi na tano(15) ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Taifa cha Utalii, Bernadetha Ndunguru akizungumza kuhusu namna bodi inavyofanya kazi yake ili kufanikisha Chuo hicho kinafikia malengo waliyojiwekea wakati wa mahafali ya kumi na tano(15) ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii. Dkt. Shogo Muzola akizungumza kuhusu mafanikio na hali ya elimu katika chuo hicho wakati wa mahafali ya kumi na tano(15) ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwakabidhi baadhi ya wahitimu wa vyeti pamoja na zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri wakati wa masomo.

 Baadhi ya wahitimu pamoja na wageni waliofika kwenye mahafali ya kumi na tano(15) ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwatunuku astashahada na Stashahada wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo katika kampasi ya Bustanini jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu 
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Utalii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad