Mtaa Kwa Mtaa Blog

MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA YAPANGWA

Droo ya Kombe la Dunia 2018 imefanyika ambapo Ureno na Hispania zimepangwa pamoja katika Kundi B.
Hiyo inamaansha Cristiano Ronaldo wa Ureno atacheza dhidi ya Hispania nchi anakochezea katika timu ya Real Madrid.
Katika droo hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Serikali wa Kremlin Palace, miongoni mwa walioudhuria ni Rais wa Urusi, Vladimir Putin na Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino.
Michuano hiyo ambayo ni mikubwa katika ngazi ya soka kuliko yote duniani inatarajiwa kuanza Juni 14 na kumalizika Julai 15, ambapo nchi 32 zitashiriki kutoka mabara matano.
Kutakuwa na viwanja 12 na miji 11 ambayo itatumika katika michuano hiyo.

Makundi yalivyopangwa haya hapa. Kundi A: Urusi, Saudi Arabia, Misri, Uruguay Kundi B: Ureno, Hispania, Morocco, Iran Kundi C: Ufaransa, Australia, Peru, Denmark Kundi D: Argentina, Iceland, Croatia, Nigeria Kundi E: Brazil, Switzerland, Costa Rica, Serbia Kundi F: Ujerumani, Mexico, Sweden, Korea Kusini Kundi G: Ubelgiji, Panama, Tunisia, England Kundi H: Poland, Senegal, Colombia, Japan
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget