HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 2 December 2017

StarsTimes kuonesha michuano ya Kombe la Dunia

Desemba Mosi ndiyo siku iliyokuwa ikisubiliwa ili kujulikana nani atakuwa kundi lipo wakati ratiba ya Kombe la Dunia iliyopangwa leo.

StarsTimes kupitia channel ya World Football  imeonyesha moja kwa moja tukio hilo la upangaji wa ratiba. Katika droo hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Serikali wa Kremlin Palace, miongoni mwa walioudhuria ni Rais wa Urusi, Vladimir Putin na Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino.

Ratiba hiyo imejumuisha timu 32 zinakazishiriki Kombe la Dunia nchini Russia.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa upangaji wa makundi ya kombe la Dunia, Meneja wa Mauzo wa Star Times, Juma Mchina Sharobaro amesema Startimes Tanzania wameamua kujikita kwenye michezo kupitia channel ya World Football ambapo zitaoneshwa mechi zote za kombe la Dunia.
 Pia aliwasisitiza watanzania kununua ving’amuzi vya Startimes kwa kuwa wamepunguza bei kwenye msimu wa sikukuu. 

"Wakati startimes wakikuwezesha kucheki kombe la dunia mwakani fanya kununua dikoda ya startimes na utapewa bonus toka princessbet kampuni ya ubashiri inayokuwezesha wewe Mteja kushinda hadi tsh milion 25 kwa siku huku ukiwa na uhuru wa kubashiri michezo tofauti kwa kiwango cha kuanzia shilingi 500 tu" alisema  Meneja Uendeshaji wa PricessBet, Jimmy Keneth.

Michuano hiyo ambayo ni mikubwa katika ngazi ya soka kuliko yote duniani inatarajiwa kuanza Juni 14 na kumalizika Julai 15 mwaka 2018, ambapo nchi 32 zitashiriki kutoka mabara matano. Kutakuwa na viwanja 12 na miji 11 ambayo itatumika katika michuano hiyo.

Makundi yalivyopangwa haya hapa.
Kundi A: Urusi, Saudi Arabia, Misri, Uruguay
Kundi B: Ureno, Hispania, Morocco, Iran
Kundi C: Ufaransa, Australia, Peru, Denmark
Kundi D: Argentina, Iceland, Croatia, Nigeria
Kundi E: Brazil, Switzerland, Costa Rica, Serbia
Kundi F: Ujerumani, Mexico, Sweden, Korea Kusini
Kundi G: Ubelgiji, Panama, Tunisia, England
Kundi H: Poland, Senegal, Colombia, Japan


Mtangazaji wa kipindi cha michezo Radio Clouds FM (Sports Extra) na Clouds TV (Sports Bar), Shaffih Dauda akizungumza jambo wakati wa kupanga makundi kwa timu zilizofuzu kucheza kombe la Dunua Nchini Urusi mwaka 2018. Meneja wa Mauzo wa Star Times, Juma Mchina Sharobaro(kulia) akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi walijinyakulia king'amuzi cha Startimes kwenye ukumbi wa Pricess Casino jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Ubashiri  ya PricessBet, Jimmy KenethMeneja wa Mauzo wa StarTimes, Juma Mchina Sharobaro akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Startimes walivyojipanga kufanya mapinduzi katika medani ya Soka leo wakati wa upangaji wa timu zilizofuzu kombe la Dunia nchini Urusi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad