HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 28, 2017

HATUNA TATIZO LA DAWA NCHI NZIMA-DKT. NDUGULILE

Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii
Serikali imesema kuwa hakuna tatizo la dawa katika sehemu kutoa huduma za afya katika Hospitali, Vituo vya Afya , Dispensari pamoja na Zahanati.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkanoge Kata ya Nyamato Wilayani Mkuranga.

Dk.Ndugulile amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa bajeti ya Wizara ya afya kumefanya Wizara kujipanga katika kuhakikisha wananchi wanapata dawa pale wanapokwenda kupata huduma za afya katika hospitali vituo vya afya, Zahanati pamoja na Dispensari.

Amesema kuwa licha na jitihada hizo serikali inakuja mpango wa kila mwananchi kuwa na bima ya afya na ni lazima na sio hiari.Dk.Ndugulile katika uzinduzi wa zahanati hiyo ameahidi kuwapelekea jokofu la kuhifadhi dawa za chanjo ili kuwapunguzia wananchi wa kufuata chanjo mbali.

Amesema Tanzania ni nchi inayoongoza katika utoaji wa chanjo duniani kwa asilimia 97.Dkt.Ndugulile ameahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili Ujenzi wa nyumba ya Mkunga katika zahanati ya Mkanoge.

Nae Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambae ni Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa jitihada za kuboresha huduma za jamii ni endelevu katika Wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Faustine Ndugulile kwa kushirikiana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga wakizindua Zahanati ya Mkanonge.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Pwani.

Mkazi wa Kijiji cha Makanonge, Themed Mkale akimkabidhi Zawadi ya Mhogo,pamoja na Mpunga Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Dk. Faustine Ndugulile.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi wa mkanoge wakati uzinduzi wa zahanati.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza juu ya harakati zilizofanyika za kujenga Zahanati ya Mkanonge.

Sehemu ya wananchi waliofika kwenye uzinduzi huu wa Zahanati ya Kijiji cha Mkanoge

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad