HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 7, 2017

CTI WAZINDUA TUZO ZA VIWANDA KWA MWAKA 2017 LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Loedigar Tenga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tuzo za The President's Manufacturer of the Year Awards 2017 kwa wanachama na wasio wanachama wa CTI na kuvitaka washiriki kujitokeza kuchukua fomu za ushiriki.




Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) limezindua tuzo za President's Manufacturer of the year awards 2017 (PMAYA) ikiwa ni mara ya 12 toka kuanzisha kwake mwaka 2005.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo za PMAYA kwa mwaka 2017, Mkurugenzi Mtendaji wa CTI Leodigar Tenga amesema kuwa tuzo hizi zinaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika kuelekea uchumi wa viwanda.

Tenga amesema kuwa tuzo hizi kwa mwaka huu zimezinduliwa mapema zaidi ili kuwapa fursa wenye viwanda kushiriki kwa wingi, kwani kuanzia mwaka 2016 tuzo za PMAYA zinajumuisha kwa wanachama na wasio wanachama wa CTI.



Akielezea tuzo zilizopita ambapo ziliweza kuleta hamasa kwa wamiliki mbalimbali wa Viwanda, Mkurugenzi Mtendaji Tenga amesema kwa mwaka 2017 anatarajia kuona namba ya washiriki ikizidi kuwa kubwa kutokana na kuruhusu pia wasio wanachama kuja kushiriki na kwa mara nyingine tena kutakuwa na tuzo ya ufanisi wa nishati.

"Kuanzia mwaka jana tumeamua kushirikisha wasio wanachama wa CTI ili kuweza kushiriki nasi katika tuzo hizi za PMAYA na hili ni jambo kubwa sana kwani tunaamini washiriki watakuwa wengi na kwa mwaka huu kutakuwa tena na tuzo ya ufanisi wa nishati, "amesema Tenga.

Kwa upande wa mdhamini mkuu wa tuzo hizo, Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa wateja kutoka benki ya CRDB Tully Mwambapa amesema mwaka huu watadhamini tuzo hizo kwa kiasi cha fedha dola za kimarekani 35,000 sawa na milioni 70 za kitanzania.

Tully amesema kuwa, benki yao imeweza kushirikiana na viwanda mbalimbali kwani benki yao inatoa mikopo kwa viwanda vidogo na vikubwa na ukiangalia kwa mwaka jana walitumia takribani bilioni 160.

Mkurugenzi Mkuu wa ISHARA Consultant Olive Mosha amesema kuwa viwanda vyote vikubwa na vidogo vinaruhusiwa kuja kushiriki katika tuzo hizo ambapo kampuni yao itasimamia kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa mashindano hayo.

Tuzo hizo zinazoratibiwa na CTI zimekuwa zinatoa mchango mkubwa sana kwa wamiliki wa viwanda kuweza kujitathmini kila mwaka kwa kuangalia wanapotakiwa kuboresha kuanzia kwenye uendeshaji wa kiwanda.
Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa wateja kutoka benki ya CRDB Tully Mwambapa akizungumza na waaandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa tuzo za The President's Manufacturer of the Year Awards 2017 wakiwa kama wadhamini wakuu wa tuzo hizo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania Leodigar Tenga.
Mkurugenzi Mkuu wa ISHARA Consultant Olive Mosha akielezea namna watakavyoweza kupata mshindi wa tuzo za The President's Manufacturer of the Year Awards 2017 na wakisisitiza washiriki kuchukua fomu mapema leo Jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wakisikiliza kwa makini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad