HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 7 December 2017

SHULE YA MSINGI TABATA YANUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA MISS UBUNGO 2014 DIANA KATO

Mkurugenzi msaidizi Sera na Mipango kutoka wizara ya maji na Umwagiliaji Paul Suley aliyekuwa anamwakilisha Katibu mkuu wa Wizara ya maji na Umwagiliaji amesema kuwa amezipokea changamoto ya shule hiyo na atawasilisha wizarani kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Shule ya Msingi Tabata ulioratibiwa na aliyekuwa Miss Ubungo 2014, Diana Kato uliogharimu takribani shilingi 613,000 za kitanzania.

Sulley alisema kuwa, amezipokea changamoto zao ikiwemo ya kutokuwa na tanki la kuhifadhia maji ataliwasilisha wizarani na pia amefurahi sana kuona wadau mbalimbali wanajitoa kwa ajili ya kusaidia jamii.

Diana Kato amesema kuwa ameweza kutoa msaada huo kwa shule ya msingi Tabata ikiwa ni katika moja ya mradi ambapo alitumia takribani kiasi cha shilingi 613,000 kwa ajili ya kulipia gharama za kuwekwa maji na kununua vifaa vya ujenzi ili kukamilisha mradi huo.
Miss Ubungo 2014, Diana Joachimu Kato akisoma risala kuhusu historia fupi kuhusu alivyoanza kutekeleza mradi wa bomba la maji safi uliokamilika na kukabidhiwa leo katika shule ya Msingi Tabata.
 Mgeni Rasmi Mkurugenzi msaidizi Sera na Mipango kutoka wizara ya Maji na Umwagiliaji, Paul Sulley  aliyekuwa anamwakilisha Katibu mkuu wa Wizara hiyo akizungumza na wanafunzi, walimu na wazazi walioudhulia uzinduzi wa bomba la maji safi katika shule ya Msingi Tabata iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni alifadhiri mradi huo Miss Ubungo 2014, Diana Joachimu Kato na kulia ni Mkuu wa Shule ya msingi Tabata, Hamisi Ngoda.
Mkuu wa Shule ya msingi Tabata, Hamisi Ngoda akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi wakati wa uzinduzi wa bomba la maji kwenye shule hiyo lililofadhiliwa na aliyekuwa Miss Ubungo Diana Kato leo shuleni hapo.
Wanafunzi wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa bomba la maji safi lililofadhiliwa na aliekuwa Miss Ubungo 2014.

Baadhi ya wazazi na wanafunzi wakufuatilia tukio la kukabidhi Bomba la maji kwenye shule ya Msingi ya Tabata, Ilaa jijini Dar es Salaam leo
Mkurugenzi msaidizi Sera na Mipango kutoka wizara ya Maji na Umwagiliaji, Paul Sulley akikata utepe kuashiria uzinduzi wa bomba la maji kwa ajili ya matuminzi mbalimbali katika shule ya Msingi Tabata leo jijini Dar es Salaam.
Picha pamoja mara baada ya kuzindua bomba la maji safi kwa ajili ya matumizi mbalimbali shuleni  hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad