HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 7 December 2017

KILIMANJARO STARS YACHEZEA KICHAPO TOKA KWA NDUGU ZAO ZANZIBAR HEROES

Mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars Eliuas Maguli (jezi nyeupe) akiwania mpira na mchezaji wa Zanzibar Heroes katika mchezo wa pili wa michuano ya CECAFA Senior Challenge leo Jijini Nairobi na kumalizika kwa Zanzibar Heroes kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

Timu ya Tanzania Bara "Kilimanjaro Stars" kupoteza mchezo wao dhidi ya Zanzibar Heroes kwenye michuano ya Cecafa Senior Challenge inayoendelea nchini Kenya Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Ammy Ninje amesema kikosi chake bado kina nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi mbili zilizobaki.

Kilimanjaro Stars iliyopo katika kundi A imebaki na michezo dhidi ya Rwanda na wenyeji Kenya ambayo Kocha Ninje anaamini watashinda na kusogea hatua ya nusu fainali.

Akizungumzia Kilimanjaro kupoteza mchezo dhidi ya Zanzibar, Kocha Ninje amesema kipindi cha kwanza timu ilicheza vizuri kiasi cha kupata goli lililofungwa na nahodha Himid Mao, lakini kipindi cha pili wakaanza taratibu na kuwaruhusu Zanzibar kurudi mchezoni hali iliyopelekea ushindi wao.

Amesema makosa mawili yaliyofanyika ndio yamewaghalimu kupoteza lakini kimpira timu imecheza mchezo mzuri.
Beki wa Kilimanjaro Stars Boniface Maganga akiwa anapambana na beki wa Zanzibar Heroes Haji Mwinyi katika mchezo wa pili wa michuano ya CECAFA Senior Challenge leo Jijini Nairobi na kumalizika kwa Zanzibar Heroes kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

"kuangalia makosa ya mchezaji mmoja mmoja Nimewaambia Wachezaji wangu wasikate tamaa bado tuna nafasi ya kufanya vizuri katika mechi zetu mbili zilizobaki,” amesema Ninje.

Kwa matokeo hayo Kilimanjaro Stars inabakiwa na pointi 1 baada ya kucheza michezo miwili katika kundi hilo la A ikisaliwa na michezo dhidi ya Rwanda “Amavubi” na wenyeji Kenya ‘Harambee Stars’.
Beki wa Zanzibar Heroes akiwa anawania mpira na mshambuliaji wa Kilimanjaro Stars Elius Maguli katika mchezo wa pili wa michuano ya CECAFA Senior Challenge leo Jijini Nairobi na kumalizika kwa Zanzibar Heroes kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad