HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 8 November 2017

Wateja wa Vodacom Tanzania na Easybuyafrica warahisishiwa huduma zao zaidi

Meneja Masoko wa huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania PLC,Noel mazoya(kushoto)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) jijini Dar es Salaam jana,Juu ya Ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya Easybuyafrica, Ambapo pamoja na mambo mengine, wateja wa Vodacom watarudishiwa 20% ya gharama za oda ya manunuzi mtandaoni wakilipa kwa M-Pesa kupitia Easybuyafrica siku ya Black Friday. Black Friday ni siku ambayo mitandao mbalimbali duniani hutoa punguzo la hadi 75% na mwaka huu itakayofanyika Nov 24. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Easybuyafrica , Moustapha Al Baghdadi na Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Jacqueline Terry.
Meneja Masoko wa kampuni ya EasybuyAfrica, Jacqueline Terry akiwaonyesha waandishi wa habari njisi ya kununua bidhaa mbalimbali kwa njia ya mtandao kupitia kampuni yao wakati wa hafla ya kusaini Ushirikiano wa kibiashara na Vodacom Tanzania PLC kwa kuwarahisishia wateja wa kampuni hiyo kulipia bidhaa zao kwa njia ya M-Pesana kupata punguzo la 20% wakilipa manunuzi ya mtandaoni siku ya Black Friday utakayofanyika tar 24 Nov. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo , Moustapha Al Baghdadi akishuhudiwa na Meneja Masoko wa huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania PLC,Noel Mazoya.
Meneja Masoko wa huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania PLC,Noel mazoya(kushoto)akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa EasybuyAfrica Moustapha Al Baghdadi(kulia) baada ya kusaini makubaliano ya Ushirikiano wa kibiashara, Ambapo pamoja na mambo mengine, wateja wa Vodacom watarudishiwa 20% ya gharama za oda ya manunuzi mtandaoni wakilipa kwa M-Pesa kupitia Easybuyafrica siku ya Black Friday. Black Friday ni siku ambayo mitandao mbalimbali duniani hutoa punguzo la hadi 75% na mwaka huu itakayofanyika Nov 24. katikati ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Jacqueline Terry.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad