HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 27, 2017

SERIKALI YAZINDUA MKAKATI WA TAIFA WA KONDOMU

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega  akikata  utepe kushairia  uzinduzi wa mkakati wa kandomu kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniania Desemba Mosi. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dr, Leornad Maboko

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, serikali imezindua mkakati wa Taifa wa Kondomu na wiki ya maonyesho na Huduma ili kuhakikisha maambukizi dhidi ya ugonjwa huu yanapungua kwa kiasi kikubwa ama kumalizika kabisa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Adallah Ulega, amesema mkakati huu umetayarishwa kueleza vipaumbele vya kimkakati vinavyohitajika kupungiza maambukizi ya VVU, Magonjwa ya ngono na mimba zisizotarajiwa
 "Takwimu za matumizi ya kondomu kwa Tanzania ni asilimia 50, matumizi haya yako chini wakati kondomu zikitumiwa kwa usahihi na mara kwa mara zinauwezo wa kupunguza maambukizi ya VVU" amesema Ulega
 Amesema mkakati huo,  unakusudia kuongeza matumizi ya Kondomu kwa wanawake na wanaume kutoka 34% kwa wanawake na 40.5% kwa wanaume ya mwaka 2012 had I 55% kwa wote ifikapo mwaka 2018.  

Aidha amesema vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 watoe taarifa ya kutumia kondomu wakati wa ngono.
"kiwango kidogo cha matumizi ya kondomu kama njia ya kuzuia magonjwa ya ngono kinatishia kufikiwa kwa malengo ya muda mrefu ya nchi tuliyojiwekea hii ikiwa ni pamoja na malengo ya dunia ya sifuri Tatu ifikapo 2030 hasa ikizingatiwa kwamba kondomu zina uwezo wa kings kwa zaidi ya 80%.
Aidha amesema, pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali, Jamii bado inamchango mkubwa katika kupambana na magonjwa ya ngono na ukimwi.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dr, Leornad Maboko akieleza jinsi maambukizi ya VVU yalivyo kwa sasa amesema, takribani watu elfu 55 kwa mwaka wanamaambukizi mapya na kundi kubwa likiwa ni vijana.  kati ya hao asilimia 40 ya vijana wanamaambukizi mapya wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.

Amesema kati ya hao asilimia 40,  asilimia 80 ni watoto wa kike.
Amesema matumizi ya kondomu yatasaidia sana maambukizi mapya ya VVU na kuwawezesha watu kuishi maisha mazuri huku wakiendesha shughuli zao.

Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani yanatarajia kufanyika desemba Mosi mwaka huu, n kitaifa yatafanyikia jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa makamu wa Rais, Samoa Suluhu Hassan.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akitembelea katika mabanda mbalimbali ya maonesho yaliyopo ndani ya Viwanja vya Mnazi Mmoja leo Jijink Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mkakati wa kandomu kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniania Desemba Mosi.
 Naibu Waziri Wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega akizungumza na taasisi mbalimbali katika uzinduzi wa mkakati wa kondomu uliofanyika leo kwenye Viwanja vyw Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri, Abdalla Ulega akielezewa namna ya kuvaa kondomu ya kiume na muelimishaji kuhusu matumizi sahihi ya kondomu kutoka T- Marc Tza Benjamin Salema alipotembelea mabanda yaliyopo ndani ya Viwanja vya Mnazi leo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad