HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 10 November 2017

MSHTAKIWA SETHI AIOMBA MAHAKAMA IMRUHUSU KWENDA KUPATIWA MATIBABU YA PUTO LAKE NCHINI AFRIKA KUSINI

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mshtakiwa Harbinder Singh Sethi,ameoimba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumruhusu kwenda kupatiwa matibabu ya puto lake lililoisha muda nchini Afrika Kusini kwa daktari wake maalumu kwa madai ya kwamba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamemueleza kuwa hawawezi kufanya upasuaji huo.

Maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo na wakili wake, Joseph Sungwa leo Novemba 10/2017 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, wakati shauri hilo linalomkabili Sethi na James Rugemarila lilipopelekwa kwa kutajwa na Mawakili wa Serikali, Vitalis Peter na Leonard Swai kudai upelelezi haujakamilika.

Katika kesi hiyo, Sethi na James Burchard Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kighushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Akiwasilisha maombi hayo, wakili Sungwa alidai alielezwa na mteja wake kwamba baada ya kufanyiwa vipimo na Muhimbili, walimweleza hawana ujuzi wa kumfanyia upasuaji wa puto.hilo na endapo litaendelea kubaki mwilini mwake linaweza kupasuka muda wowote na kuzalisha sumu ambayo litaatarisha maisha yake na njia pekee iliyobakia ni kwa mshtakiwa Sethi kumuona daktari wake anayeishi Afrika Kusini.

“Ili mshtakiwa aweze kuja mahakamani kuudhuria kesi yake na hatimae kuweza kujitetea, tunaomba kama inawezekana aende kumuona daktari wake ambaye anaishi Afrika Kusini kwa matibabu”, alidai Sungwa.

Ombi hilo lilipingwa vikali na wakili wa serikali,Swai akidai Muhimbili haijashindwa kumfanyia upasuaji wa puto mshitakiwa huyo, bali anajicheleweshwa mwenyewe kutokana na kutaka uwepo wa daktari wake wa Afrika Kusini.

Swai alidai kwa taarifa kutoka magereza ambako mshtakiwa ndiko anaishi imedai repoti kutoka Muhimbili ilisema kuwa inaouwezo wa kumfanyia operesheni mshtakiwa lakini mshtakiwa mwenyewe anahitaji daktari wake aliyeko Afrika Kusini ndiye aje kumtibu.

“Tanzania tunao madaktari jambo hili la kumleta daktari kutoka nje ya nchi linahitaji kufuata taratibu na litahusisha taasisi za mbali mbali ikiwemo serikali ili kumruhusu daktari wake aje nchini kumtibu” amedai Swai.

Akielezea juu ya upelelezi Swai alidai wapo katika hatua nzuri na wanataka kwenda mahabusu kuchukua maelezo ya onyo ya washitakiwa na iwapo amri ikitoka wachunguzi wataenda kuchukua maelezo yao.Hoja ya upelelezi iliibuliwa na Wakili Michael Ngalo,aliyedai upelelezi umechukua muda mrefu ni takriban miezi mitano saaa haujakamilika na washitakiwa wapo mahabusu.

Baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili, Hakimu Shaidi alisema juu ya mshitakiwa kama anawezo wa kutibiwa Muhimbili ama la, mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri yoyote hivyo wawasilishe maombi Mahakama Kuu.

Kesi hiyo imeahihirishwa hadi Novemba 24, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad