HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 13, 2017

JUKWAA LA AFYA LA DICOTA LAFANA, GREENBELT, MARYLAND


Meza kuu kutoka kushoto ni Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Mhe. Wilson Masilingi, Naibu Waziri wa afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman,Mkuu wa kitengo cha Diaspora Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika Mashariki, Balozi Anisa  Mbega, Bi.Adila Hilal Vuai mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) !, Bwn. Assenga kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Dr. Ali Salum Ali Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. wakifuatilia jukwaa la afya lililoandaliwa na DICOTA katika kuwakutanisha wadau wote nje na ndani ya Marekani sekta ya afya kuwatambua na kuthamini mchango mkubwa wanaotoa katika sekta hiyo nchini Tanzania. Jukwaa la afya lilifanyika siku ya Jumamosi Novemba 11, 2017 Martins Crosswind Greenbelt, Maryland nchini Marekani. Picha naVijimambo Blog na Kwanza Production
Bwn. Lunda Asmaniakiwakaribisha wadau wote na akifungua jukwaa la afya.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akisoma hotuba yake kwenye kongamano la Afya lililofanyika siku ya Jumamosi Nov 11, 2017 Greenbelt, Maryaland nchini Marekani. Katika hotuba hiyo aliwashukuru DICOTA kwa kuandaa jukwaa hilo la wadau wa afya kwa kthamini kazi kubwa inayofanywa na wadau hao na jitihada binafsi zinazofanywa kwa kusaidia ndungu zao nyumbani Tanzania pia alisema Rais Dkt John Pombe Magufuli anatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Diaspora kwa nchi yao.
Balozi wa African Union nchini Marekani, Mhe.Arikana Chihombori Quao akichangia kwenye jukwaa hilo na kueleza changamoto nyingi nchi za Afrika inazopata katika sekta hiyo kutokana namiundo mbinu kuwa duni na sababu kubwa ni jinsi wakoloni walivyoligawa bara la Afrika na kuwa nchi mbalimbali kwa kuogopa nguvu ya Afrika na utajiri wake usije ukaongoza Dunia.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman akiwashukuru Diaspora kwamchango mkubwa kwa sekta ya afya Zanzibar na baadae kutoa salamu za Rais wa Zanzibar Mhe. Dr Ali Mohamed Shein kwa kutoa shukurani zake kwa kuthamini mchango mkubwa wa Diaspora hasa katika sekta ya Afya.
Balozi Anisa Mbega mkuu wa idara ya Diaspora Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akishiriki jukwaa la Afya kwa kuwapongeza DICOTA kwa kuandaa jukwaa hilo na kuwakutanisha wadau wa afya na Serikali inathamini na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Diaspora.
Balozi Liberata Mulamula akitoa shukurani zake kwa DICOTA kwa kuandaa jukwaa la afya na baadae kutoa mfano wa mtu akiwekewa fedha na afya bora yeye atakimbilia kwenye fedha bila lutambua bila afya njema hata hizo fedha hataweza kudumu nazo kwa maana kwamba binadamu wengi hawaelewi umuhimu wa afya lazima tutambue hilohuku akitoleamfano mwingine wa nyani unapo muwekea fedhana ndizi yeye atachangau ndizi kwa sababu anajua bila ndizi maisha yake yapo hatarini. 
Dr. Mary Banda akielezea jinsi alivyotumia elimu yake kwa kuelekeza nguvu yake kusaidia sekta ya afya mkoa wa Kagera.

Bi. Christine


Bi. Adila Hilal Vuai mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) akitoa shukurani kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa jitihada za Diaspora katika sekta ya afya Zanzibar na kuwapongeza DICOTA kwa kuandaa jukwaa la Afya na kuwaasa kutumia lugha ya Kiswahili katika kuendeleza na kuthamini utamaduni wetu.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad