HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 13, 2017

BENKI YA KILIMO YATUPIA JICHO MIRADI YA KILIMO ZANZIBAR

 Katika jitihada za kuchagiza maendeleo ya kilimo Visiwani Zanzibar, Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanya ziara katika miradi mbalimbali ya kilimo visiwani humo.

Ziara hiyo imelenga kufanya utambuzi wa miradi ambayo ina uhitaji wa mikopo ya gharama nafuu hali itakayochochea kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma zisizo za kifedha kwa wakulima kama vile kujengewa uwezo juu ya uandaaji wa andiko la miradi ya Kilimo, upatikanaji wa taarifa za masoko, usimamizi wa biashara, mafunzo juu ya miradi ya Kilimo na mbinu za majadiliano ya mikataba.

Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Zanzibar (ZSTC) ambao walikuwa wenyeji wa TADB, Bw. Ussi Mohamed Juma (aliyesimama) akizungumza na ugeni huo. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya ZSTC Kinazini, Zanzibar. 

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi hiyo, Bibi Rehema Twalib, amesema kuwa TADB ikiwa chombo cha Muungano ina wajibu kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania hasa katika kuchagiza mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya  asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.

“Ziara yetu hii inalenga katika kusaidia juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo,” alisema.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Bibi Rosebud Kurwijila, Bibi Rehema Twalib, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo (aliyesimama), akizungumza wakati wa kikao na uongozi wa ZSTC. 
Akizungumza na ugeni huo, Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Zanzibar (ZSTC) ambao walikuwa wenyeji wa TADB, Bw. Ussi Mohamed Juma alisema ujio wa TADB visiwani humo kutasaidia wakulima wa  Zanzibar ambao kama walivyo wakulima wengine nchini kukosa mikopo ya gharama nafuu hali inayorudisha nyuma jitihada za wakulima hao.

Akaongeza kuwa lengo la TADB linasadifu majukumu ya kuanzisha kwa ZSTC ambayo yanalenga kuchagiza maendeleo katika mnyororo mzima wa ongezeko la thamani katika mazao ya ili kilimo hivyo kukuza, kuboresha ubora na kuongeza ushindani wa kupamba na bidhaa nyingine za kilimo katika soko la dunia.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (alyesimama) akifafanua kuhusu malengo ya TADB wakati wa mazungumzo yao na ZSTC. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya ZSTC Kinazini, Zanzibar. 
Bw. Juma akaahidi ZSTC kutumia ushirikiano huo na TADB katika kuwezesha maendeleo na kusaidia mabadiliko ya sekta ya kilimo visiwani humo.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa ujio wa TADB visiwani Zanzibar utasaidia kutatua tatizo la mitaji kwa wakulima kwani kwa sasa taasisi za nyingi za fedha zinaelekeza mikopo zaidi kwenye upande wa biashara na bidhaa.

“Hali ya ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara na bidhaa na kuwasahau wakulima na wasindikaji wa mazao, hivyo tunaamini TADB itasaidia kutatua changamoto hii,” alisema.
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha (aliyesimama) akizungumzia fursa za mikopo inayotolewa na Benki hiyo wakati wa mazungumzo yao na ZSTC. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya ZSTC Kinazini, Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe wa Ugeni kutoka TADB wakifurahia maji ya madafu walipotembelea Kambi ya Jeshi ya Kujenga Uchumi (JKU), Machui Zanzibar. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga. Wengine pichani ni wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Bw. Simon Migangala (kati) na Bw. Hussein Mbululo (kulia).
Mkuu wa Kambi ya Jeshi ya Kujenga Uchumi (JKU), Machui, Zanzibar, Kapteni Makame Kombo (kushoto) akieleza shughuli za uzalishaji kupitia kilimo zinafanywa kambini hapo.
Afisa Misitu na Maliasili Zisizorejesheka kutoka Idara ya Kilimo Zanzibar, Bw. Badru Kombo Mwamvura (katikati) akitoa ufafanuzi wa zao la karafuu kwa ugeni kutoka Benki ya Kiimo Tanzania wakati walipotembelea Shamba la Mikarafuu la Serikali lililopo Kizimbani, Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad