HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 29 November 2017

Jinsi ya Kuajiri Mtendaji Mkuu Ndani ya Siku 5Katika soko la ajira Tanzania, vipaji hutokea na kutoweka kila mara. Hivyo unaweza kuta kampuni yako inakosa kipaji muhimu katika muda ambao unakihitaji. Unakuta unataka kuajiri haraka lakini hutaki kupata mtu asiyefaa.
Je Utafanyaje? Utafanya nini ili kuajiri mtu anayefaa na kwa haraka.

Punguza Hatua za Usaili

Kampuni nyingi huulizia wadhamini pale tu muombaji anapokuwa amefaulu usaili wa hatua ya kwanza. Inaweza kupita siku kadhaa mpaka muombaji akupatie taarifa hizo. Epuka kupoteza muda huu kwa kuomba taarifa hizi wakati wa maombi ya awali, na kuita kwenye usaili waombaji ambao wadhamini wao wametoa maoni mazuri.

Andika Maelezo ya Kazi Vizuri

Maombi mengi ya kazi hukosewa kwa sababu maelezo yaliyokuwa kwenye tangazo la kazi hayakujitosheleza. Kuepukana na hili hakikisha umeweka maelekezo yote ya muhimu kwenye tangazo lako la kazi. Pia hakikisha umepangilia vizuri tangazo lako ili kuvutia waombaji wenye sifa na ili kufanya lieleweke kwa urahisi. Unaweza kutumia tovuti kama BrighterMonday, hii inakusaidia kupangilia tangazo lako na kulifikisha kwa waombaji wengi. Pia tovuti kama hizi huwa zina huduma ya kulikuza tangazo lako ili lifikie watu wengi zaidi.

Pandisha Cheo Badala ya Kuajiri

Kutangaza nafasi ya kazi ndani ya kampuni lako kutasaidia kuwakuza wafanyakazi wako, hii itawahamasisha wafanye kazi kwa juhudi zaidi. Faida kubwa ya kufanya hivi ni kwamba mfanyakazi wako tayari unamjua, unajua uimara na udhaifu wake. Na yeye tayari anaijua biashara yako, hivyo hautatumia muda mwingi kumfundisha kazi.

Tumia Mtandao wa Wafanyakazi Wako

Waambie wafanyakazi wako pale ambapo kuna nafasi. Kwa kutumia mtandao wa marafiki na familia za wafanyakazi wako unaweza kupata mtu mwenye sifa kwa haraka na kwa urahisi. Faida ya kufanya hivi ni kwamba mtu utakaye muajiri, itakuwa ni rahisi kwake kuelewana na wafanyakazi wenzake.

Ajiri Kampuni ya Rasilimali Watu

Kampuni za rasilimali watu ni chaguo zuri, lakini mengi ya makampuni hayo hutoza gharama kubwa pamoja na asilimia ya mshahara kwa kila nafasi ya kazi. Pia inachukua muda kutafuta kampuni inayokufaa.

Sasa kuna mpinzani mpya kwenye soko la ajira. BrighterMonday ni tovuti ya ajira inayoongoza  Tanzania. Wafanyakazi wake waliobobea hutumia tovuti hiyo pamoja na mitandao yao yenye waombaji waliosajiliwa zaidi ya 98,000. BrighterMonday inapitia maombi yote na kukupatia orodha fupi ya watu watakaokufaa. Na inafanya yote haya ndani ya muda mdogo iwezekanavyo na kwa gharama nafuu.

Watu husema, mali kubwa ya kampuni yako ni wafanyakazi wake. Ajiri Sasa!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad