HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 13, 2017

WANAFUNZI WAASWA KUNAWA MIKONO WATOKAPO MSALANI.

 Wanafunzi wa shule ya msingi Mkwawa na Mabibo wakiwa katika maadhimisho ya unawaji mikono ambayo hufanyika Oktoba 13 kila mwaka.

SHULE mbili za manispaa ya Kinondoni zaadhimisha siku ya unawaji mikono ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba 13 ikiwa na kaulimbiu ya mikono safi kwa manufaa ya sasa na ya baadae.

 Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta amesema kuwa kila mtoto anatakiwa kunawa mikono kabla na baada ya kula pamoja na watokapo masalani ili kuepukana na maradhi ya kipindupindi na maradhi yaletwayo kwa kula uchafu.

Amesema kuwa siku hii ni muhimu hasa kwa watoto wanaokurupuka kumegeana vyakula au vitafunwa wawapo shuleni bila ya kunawa mikono yao na bila ya kujua ni nini madhara ya kula bila kunawa.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya kunawa mikono iliyofanyika katika shule ya Msingi Mabibo na shule ya Msingi Mkwawa jijini Dar es Salaam leo.
Pia amewaasa wanafunzi wa shule za msingi Kigogo pamoja na Mkwawa kunawa mikono mikono kila wanapotaka kula na baada ya kula pia marabaada ya kutoka maeneo ambayo wanashika uchafu.
 Wanafunzi wa shule ya Msingi Kigogo na shule ya msingi Mkwawa wakiwa katika siku ya kunawa mikono iliyoadhimishwa shuleni hapo kwaajili kuelewa manufaa ya kunawa mikono kabla ya kula, baada baada ya   kula,  na baada ya kutoka msalani kwaajili ya kujikinga na maradhi yanayoletwa na kuto kunawa mikono.
 Wanafunzi wa chuo kikuu cha Muhimbili wanaosoma maswala ya mazingira na afya wakiwasomea watoto jinsi ya kujilinda na maradhi yatokanayo na kuto kunawa mikono.
 Mwanafunz wa chuo Kikuu cha Muhimbili Kerobe  TEHSA akiwafundisha watoto jinsi ya kunawa mikono kwa kutumia kibuyu chirizi ambacho ni rahisi zaidi kuliko kuchota maji kwa kutumia kikombe ambayo ni kwaajili ya kunawa mikono kabla na baada ya kula na wakati watokapo msalani hii ikiwa ni siku ya unawaji Mikono iliyoambatana na kauli mbiu ya Mikono safi kwa manufaa ya sasa na yabaadae.

 Afisa elimu Sayansikimu manispaa ya Kinondoni, Martha Kussaga akizungumza wakati wa kuadhinishi siku ya unawaji mikono iliyofanyika katika shule ya msingi Mkwawa na Kigogo jijini Dar es Salaam leo.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akiwazawadia walimu wakuu wa shule za msingi Mkwawa na Mabibo sabuni kwaajili ya waafunzi kuzitumia kunawa mikono wawapo shuleni kila watokapo chooni hii ni kwaajili ya kuadhimisha siku ya unawaji wa mikono ambayo hufanyika kila Oktoba 13 kila mwaka duniani kote.
Afisa usafi wa Manispaa ya Kinondoni, John Kijumbe akizungumza na wanafunzi pamoja na waalimu katika siku ya maadhimishoya Unawaji Mikono ambayo hufanyika kila Oktba 13 kila mwaka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad