HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 13 October 2017

MTANDAO WA WANAWAKE WENYE ULEMAVU TANZANIA WAZINDULIWA LEO.

WANAWAKE wenye ulemavu Tanzania wamezindua mtandao wa wanawake wenye ulemavu Tanzania ambao utakuwa ukiwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtandao huo jijini Dar es Salaam leo 
Katibu wa jumuiya ya wanawake na watoto wenye ulemavu Tanzania na diwani manispaa ya Ilala, Nuru awadhi amesema kuwa mtandao huo utakuwa karibu zaidi na wanawake walemavu wa Tanzania ili kujua changamoto za kiuchumi zinazo wakabiri.

 Mtandao huo ambao upo chini ya mwavuli wa shirikisho la watu wenye ulemavu tanzani(SHIVYAWATA) amaesema kuwa mtandao huo utalenga zaidi katika kuwainua kiuchumi wanawake walemavu pamoja kuwasaidi kupata mikopo mbalimbali kutka taasisi za kifedha ambazo zitajitokeza kuwasaidi kutokana na hali zao. 
Katibu wa jumuiya ya wanawake na watoto wenye ulemavu Tanzania na diwani manispaa ya Ilala, Nuru awadhi akizungumza na wanawake walemavu wakati wa uzinduzi wa Mtandao wa wanawake wenye ulemavu ambapo wanakauli mbiu ya Fursa kwa wanawake wenye ulemavu ni chachu ya maendeleo.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtandao wa wanawake walemavu amesema kuwa ''Nia yetu ni kuwaunganisha wanawake walemavu ili kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili".
 
Mbunge wa viti maaluum wa watu wenye ulemavu, Amina Moleli akifungua pazia kwaajili ya uzinduzi wa mtandao wa wanawake nyenye ulemavu Tanzania  uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake na watoto wenye ulemavu Tanzania, Doris Kulanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtandao wa wanawake wenye ulemavu jijini Dar es Salaam leo. amesema kuwa  mtandao huo utasaidia kupunguza changamoto mbalimbali zinazo wakabiri wanawanye wenye ulemavu kwa kushirikiana pamoja na kupendana ili kuleta mabadiliko yaliyo na tija kwa wanawake.
Katibu wa jumuiya ya wanawake na watoto wenye ulemavu Tanzania na diwani manispaa ya Ilala, Nuru awadhi akijibu swali kutoka kwa mwanachama wa mtandao wa wanawake wenye Ulemavu Tanzania hayupo Pichani katika uzinduzi wa mtandao huo jijini Dar es Salaam leo.
Mbunge wa viti maaluum wa watu wenye ulemavu, Amina Moleli akizungumza na wanachama wa mtandao wa wanawake wenye ulemavu tanzania jijini Dar es Salaam leo.
 

Baadhi ya wanawake walemavu wakichangia mada katika uzinduzi wa Mtandao wa wanawake walemavu jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad