HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 13, 2017

Ecobank yaweka wazi mikakati ya kuhudumia wafanyabiashara barani Afrika

Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya mkutano wa biashara uliondaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake pamoja na wadau wengine wa sekta ya fedha. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akizungumza  na baadhi ya wateja wa benki hiyo jana jijini Dar es Salaam baada ya mkutano wa biashara uliondaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake pamoja na wadau wengine wa sekta ya fedha.

Ecobank imeeleza  mikakati  yao kutoa huduma bora kwa wateja wake na wafanyabiashara nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla huku ikitoa wito kwa wateja wote kuendelea kufurahia huduma bora  za kibenki zinazotoa ufumbuzi kwa mahitaji mbalimbali yakiwemo yale yanayohusu malipo kwa kuwa huduma zao zinauwezo wa kuvuka mipaka ya nchi kwa kuwa mtandao wao umeendea na unauwezo wa kuhudumia  Afrika na duniani kote

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee wakati wa mkutano wa kibiashara ambao uliandaliwa na benki hiyo na kuhusisha wateja pamoja na wadau wengine wa benki hiyo.

Alisema Ecobank inatoa ufumbuzi wa kipekee wa biashara ya intra-Afrika, na kuwezesha wateja wake kukabiliana na biashara zao za kimataifa kwa ufanisi na kupunguza upotevu wa malipo pamoja na kufanya kazi kwa ukaribu na wateja katika maeneo muhimu kama vile kushughulikia Malipo, Usindikaji, mambo yanayohusu Makazi, mambo ya kifedha, kupunguza upotevu wa fedha pamoja na kuimarisha mikopo.

Kuhusu suluhisho la biashara ya kifedha alisema, "Wateja wanafaidika kutokana huduma za  mikopo barani kote ambako benki hiyo ina matawi kwenye nchi 33."

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo, wateja wanapata muda muafaka kwa uharaka na urahisi wakati wa kupata huduma kama kuagiza LCs, makusanyo ya kutoka nje ya nchi, dhamana kwa bidhaa za wateja, Export LCs (kushauri na kujadili), makusanyo ya kutoka nje ya nchi, kuwekewa dhamana, dhamana ya utendaji, huduma za kibiashara barani Afrika, makusanyo ya kikanda pamoja na Malipo ya Kimataifa.

"Lengo la Ecobank ni kutoa huduma za kipekee kwa wateja watu huku pia tukiimarisha ushirikiano wa kifedha barani Afrika na kutoa ufumbuzi wa kuwezesha wafanya biashara katika maeneo mbalimbali. Huduma za kibiashara za Ecobank huwawezesha  wafanya biashara nje ya nchi kupata dhamana ya malipo bila haja ya Barua ya Mikopo na gharama zake zinazohusiana na muingizaji, "alisema Bi Mzee.

Alisema Ecobank ikiwa kwenye pande zote mbili za kibiashara, wateja wanafaidika kutokana na suluhisho la mwisho la kukamilika na kuongeza kwa ukusanyaji wa fedha kikanda  na pia huwapa fursa wafanyabiashara kupata papo kwa uhamisho chini ya dola 10 000 huduma ambayo inaruhusu fedha kuhamishiwa kote barani Afrika na kupata pesa ya papo hapo.

"Ikiwa inapatikana kwenye nchi 33 za Afrika - zaidi ya benki yoyote duniani - Washirika wa Ecobank wanaweza kuthibitisha na kujadili Barua ya Mikopo kwa wateja katika nchi hizo, na pia kusimamia malipo yanayohusiana na biashara kutoka kwa mabenki nje ya Afrika," alisema

Bi Mzee aliwaambia wadau na wateja kwenye mkutano huo kwamba Ecobank pia inatoa huduma ya kifedha wakati wa kuagizwa kwa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi, huduma ya kifedha wakati wa kusafirishwa kwa bidhaa na huduma nje ya nchi, huduma za kifedha wakati wa kusafirisha bidhaa au mizingo, na kurahishiza Malipo ya Ankara na haya yote yanafanyika ili kuokoa muda na kupoteza rasilimali zaidi.

Mkutano huo pia ulitoa nafasi kwa wateja na wadau mbalimbali wa benki hiyo na kuweza kutoa maoni na pongezi zao   kwa benki hiyo.

Akizungumzia juu ya mkutano huo, mmoja wa mteja wa benki hiyo......, alisema, "natoa shukrani za dhati kwaa Ecobank kwa fursa hii ambayo wametupa kwa sababu tumejifunza mambo mengi kuhusu masuala ya kifedha na hasa pale tunapofanya biashara nje ya nchi yetu.

"Hii ni hoja na mpango mzuri sana kutoka kwa Ecobank Tanzania. Kuonyesha kumjali mteja binafsi kama sisi kunachochea na kuongeza uhusiano uliopo kati yetu sisi na benki. Mbinu hii imekuwa suluhisho linapokuja kushughulikia mahitaji yetu na tunafurahi sana na huduma zao. "Aliongeza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad