HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 13, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE: KAZI ZA SANAA YA UFUNDI SIO YA WATU WASIOKWENDA SHULE

 Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wasanii wa shirikisho la sanaa za ufundi Tanzania pamoja kuwapongeza kwa kazi za mikoni wanazozifanya wasanii hao leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Naibu waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo Juliana Shonza, akizungumza na wandishi wa habari pamoja na wasanii wa shirikisho la sanaa za ufundi Tanzania na kuwataka( BASATA) kuendelea kuinua vipaji vya wasanii hapa nchini hasa kwa wale walioko wa mikoani.
Wageni waalikwa waliojitokeza kwa wingi katika kuhudhuria mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa maigizo ya maonyesho ya  jukwaani wakifanya igizo linalohusu kampeni ya kuzuia rushwa  leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.

Na Agness Francis ,Blogu ya jamii
Waziri wa habari,utamaduni, sanaa na michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amehudhudhuria  mkutano   wa  wasanii wa shirikisho la sanaa za ufundi  hapa nchini kusikiliza maendeleo na changamoto zinazowakabili wasanii hao na kuwataka kuchangamkia fursa kazi za mikono yao.
Katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Shirikisho hilo la sanaa za ufundi  hapa nchini ambalo lilianza rasmi mwaka 2009 na kupata usajili wake mwaka 2010 ambapo wasanii hao walimepata mafanikio  kwa kushirikiana na (BASATA)pamoja na ubalozi wa China katika mradi ambao ulijulikana kwa jina la Tingatinga Art Biennale na walipatikana washindi wawili ambao walizawadiwa tiketi ya kwenda nchini China.
Vile vile shirikisho limeeleza changamoto zinazowakabili wasanii hao kuwa Elimu ya sanaa za ufundi haifundishwi  mashuleni, hakuna kituo maalumu  cha Taifa cha kuonesha kazi za wasanii na masoko ya sanaa kuwa hafifu kutokana na ugumu wa usafirishaji wa vinyago kwenda  nje ya nchi kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
Aidha Waziri Mwakyembe amekanusha dhana potofu isemwayo  kuwa wasanii wa sanaa za ufundi wengi wao  hawajaenda shule na amesema kuwa wizara yake itaunga mkono na kushirikiana bega kwa bega  na juhudi za  sanaa hiyo ili kuepukana na wanyonyaji wa  kazi ya wasanii hao.
Nae naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Juliana Shonza amemalizia kwa kutoa wito kwa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) kuendelea kuinua vipaji  kwa kuweza kuwafikia hasa  wasanii wa mikoani  na wilayani ambao wamesahaulika kwa muda mrefu katika kuiendeleza tasni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad