HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 3 October 2017

TUNASUBIRI MASAA 48 TUJUE MAENDELEO YA NGOMA- DAKTARI


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Baada ya kuumia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma na kushindwa kufanya mazoezi jana pamoja na kikosi kutokana na maumivu ya misuli siku ya Jumamosi.

Ngoma baada ya kuumia hakuweza kurejea tena uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi, siku ya  jana hakufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenginena kupewa mapumziko na daktari wa timu Hussein Bavu.

Ngoma alipewa saa 24 hadi 48 za uangalizi chini ya daktari wa Yanga ili kuona maendeleo kabla ya kutoa majibu kama anaweza kurudi uwanjani mapema au vinginevyo.

Dakatri wa timu hiyo Bavu amesema kuwa baada ya masaa 24 hadi 48 ndipo wanaweza kutoa majibu sahihi kwani kwa sasa wamempa mapumziko Ngoma ili aweze kurejea katika hali ya kawaida na kuangalia maendeleo yake.

Kwa sasa maendeleo ya Ngoma yanaendelea vizuri na anatembea vizuri ukilinganisha na ilivyokuwa mwanzo, anaweza kufanya mazoezi binafsi ikiwa ni tiba ya jeraha lake

Yanga inakabiliwa na mchezo wa raundi ya sita ya ligi kuu VPL dhidi ya Kagera Sugar October 14, 2017 kwenye uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad