HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 3 October 2017

VIJANA KATA YA BUZA WAUNGANA KUPAZA SAUTI KATIKA KULETA MAAENDELEO HAPA

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
Vijana wa kata ya Buza katika  mtaa wa Kidagaa wamejitokeza kwenye semina ya mafunzo  ya kujiunga na taasisi ya sauti ya vijana (MYIDC) Temeke  ili kuepukana na changamoto za kukaa mitaani bila kazi maalumu ya kufanya .

Nae Mwenyekiti Mtendaji  MYIDC,  Ismae  Mnikite amesema hayo  katika semina hiyo iliyofanyika mtaa wa Kidagaa  kata ya Buza  halmashauri ya Temeke  amesema kuwa lego la mafunzo hayo ni kutaka kuwafanya vijana waweze kuunda jukwaa la vijana na  baada ya hapo watapatiwa mafunzo kuhusu dira ya vijana na pia lengo likiwa ni kupaza sauti zao katika kuleta maendeleo.

Naye mkazi wa Buza kata ya Kidagaa Fatma Ramadhani  amesema kuwa amepata mwamko huo wa kijiunga  na taasisi hii ya sauti ya vijana (MYIDC) ili kuepukana na changamoto ya kukaa  tu mitaani ameona ni vizuri kutumia fursa zinazotolewa kama kujiunga katika vikundi vya ujasiliamani ili kujikwamua kiuchumi hapa Nchini.

Mkazi mwingine naye Rajabu Charz amesema kuwa  katika mafunzo hayo amejifunza  namna ya kutafuta na kuweka mtaji kwa ajili ya kuanzisha biashara na kuondoa woga wa   kuthubutu katika kafanya jambo la kuleta mafanikio.
 Mwenyekiti Mtendaji  MYIDC,  Ismae  Mnikite akizungumza na waandishi wa habari pamoja na vijana wa mtaa wa Kidagaa kuhusu umuhimu wa mradi wa Sauti ya Vijana (MYID) katika kata ya Buza mtaa wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 Muwakilishi wa Diwani kata ya Buza, Mahmoud Rashidi akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu changamoto  zinazowakabili vijana na kujitahidi kujitokeza kwenye shuhuli kama hizi  kutokana na  kuwa na utayari, pia amewapongeza vijana wa kata hiyo kwa kujitokeza  kuhudhuria mafunzo hayo katika kata ya Buza mta wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 Mkazi wa  Buza  kata ya Kidagaa, Fatma Ramadhani akizungumza na waandishi wa habari kususu kuchangamkia fursa na kutoa pongezi za dhati kwa sauti ya vijana  MDYDC kwa kuona umuhimu wao kama vijana Taifa la kesho katika kata ya Buza mta wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar Es Salaam.
 Mkazi wa kata ya Buza mtaa wa Kidagaa, Rajabu Charz akizungumza na waandishi wa habari katika kata ya Buza mta wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke akitoa wito kwa vijana wenzake kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza  hapa Nchini.
Wakazi wa kata ya Buza mtaa wa Kidagaa waliojitokeza kuhudhuria semina ya mafunzo yaliyotolewa na Mradi wa sauti ya vijana MYIDC ikiwa lengo ni kupata sauti ta vijana pale inapotakiwa kufika ili kuleta maendeleo hapa Nchini.Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad