HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 30 September 2017

PROF. MAGHEMBE AFUNGUA SIKU YA UTALII DUNIANI INAYOFANYIKA KITAIFA MKOANI IRINGA, ATOA WITO KWA WANANCHI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA VITA DHIDI YA UJANGILI NCHNI

Na Hamza Temba-WMU
...............................................................
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe tarehe 30 Septemba, 2017 amefungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na Serikali katika kupambana na Majangili kwa kutoa taarifa za siri zitakazoweza kuwaibaini na kuchukuliwa hatua.

“Ili kulinda uwepo wa rasilimali za utalii zilizopo kwa vizazi vya sasa na vijavyo, ni lazima wananchi kushirikiana pamoja na Serikali katika mapambano dhidi ya ujangili, mkiona mtu ananyemeleanyemelea huko porini tuambieni tutamshukia kama mwewe, hizi rasilimali na zetu sote” alisisitiza Prof. Maghembe.

Alisema changamoto ya ujangili bado ipo katika baadhi ya maeneo hapa nchini, alitaja maeneo hayo kuwa ni upande wa Pori la Rugwa na Selous karibu na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo watu huingiza mifugo hifadhini kwa kisingizio cha kutafuta malisho wakati huo huo wakifanya uhalifu wa kuua tembo.

Prof. Maghembe alifungua maadhimisho hayo pamoja na Maonesho ya Karibu Kusini na maonesho ya wajasiariamali wa viwanda vidogo SIDO yaliyoshirikisha wajasirimali kutoka mikoa ya nyanda zajuu kusini kwa lengo la kuonesha bidhaa zao zitakazoweza kutumiwa na watalii pamoja na watoa huduma hiyo. 

Akifungua maadhimisho hayo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Prof. Maghembe alisema, kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu kwa upande wa Siku ya Utalii Duniani ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo wakati ile ya Maonesho ya Karibu Kusini ikiwa ni “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.

Alisema sekta ya utalii imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi kwa kuchangia asilimia kubwa ya mapato ya Serikali, kuongeza ajira, kipato cha jamii na kuchochea ukuaji wa sekta zingine. 

"Utalii ndio ndio sekta pekee inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha za kigeni kwa asilimia 25, Aidha, inachangia asilimia 17.5 ya pato la taifa na asilimia 11 ya ajira zote nchini" alisema prof. Maghembe. 

Alisema mapato yanayotokana na utalii yameongezeka kutoka Dola za Kimarekani milioni 1,353.29 mwaka 2011 hadi Dola za Kimarekani milioni 2,131.57 mwaka 2016.

Alisema mchango huo umechagizwa na ongezeko la watalii kutoka nje ya nchi ambao waliongezeka kutoka 867,994 mwaka 2011 na kufikia 1,284,279 mwaka 2016.

Hata hivyo, alisema mafanikio hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na juhudi za Serikali katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali, utangazaji, mazingira bora ya uwekezaji na ushirikiano madhubuti baina ya sekta ya umma na binafsi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani alisema Serikali imekusudua kuhakikisha kuwa utalii wa nyanda za juu kusini unakua juu zaidi uweze kutoa mchango stahiki kwenye pato la taifa. Alitoa wito kwa wananchi kutunza vivutio vya utalii vilivyopo, kuhifadhi mazingira na kupiga vita ujangili.

"Kwa upande wa sekta binafsi na wananchi kwa ujumla natoa witoe washirikiane na Serikali kuweka mazingira bora na ya kuvutia katika maeneo yenye vivutio  vya utalii ikiwemo hoteli za kisasa kwa ajili kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi kutembelea vivutia hivyo" alisema Mhandisi Makani.

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina masenza alisema katika kuunga mkono azma ya Serikali ya kukuza na kufungua utalii wa Nyanda za Juu Kusini Serikali ya mkoa wake kwa kushirikiana na wadau wa utalii wameandaa Mpango Makakati wa kukuza sekta hiyo mkoani humo. Mpango huo umezinduliwa jana na Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe.

Kila mwaka nchi wanachama wa Shirika la Utalii Duniani huadhimisha Siku ya Utalii tarehe 27 Septemba kwa lengo la kuhanasisha umuhimu wa sekta hiyo katika kuleta maendeleo ya jamii, utamaduni, kukuza demokrasia, kutunza na kuhifadhi mazingira, kujenga uchumi na kuimarisha mahusiano ya kitaifa na kimataifa. Kilele cha Maadhimisho ni siku ya jumanne tarehe 2 Oktoba, 2017.
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (katikati),  Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) wakiimba wimbo wa Taifa katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe, akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 2, Oktoba. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani akizungumza katika maadhimisho hayo mkoani Iringa jana.
Mkuu wa Wilaya ya Iirnga, Richard Kasesela akiratibu shughuli nzima ya maadhimisho hayo.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mkakati wa Utalii wa Mkoa wa Iringa ambao umeandaliwa kwa lengo kuunga mkono azma ya Serikali wa kufungua utalii wa Nyanda za Juu Kusini katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Amina Masenza na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto), Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wa Serikali wakionesha Mkakati wa Utalii na Jarida la Iringa baada ya uzinduzi rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga akiwa na baadhi ya washiriki wengine kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo.
 Baadhi ya Machifu wa Iringa waliohudhuria ufunguzi wa maadhimisho hayo.
 Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatila ufungunguzi wake.
Sehemu ya washiriki wa maadhimisho hayo ya Wiki ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini. Nyuma yao ni mabanda ya maonesho hayo.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakielekea kukagua mabanda ya maonesho katika viwanja vya Kichangani Mkoani Iringa jana.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akipimwa afya katika banda la MSD wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. KKauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni  “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto), akikagua bidhaa za wajasiriamali wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa pili kushoto). 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza moja ya bidhaa za wajasiriamali wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatu kulia). Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), akikagua kifaa maalum cha kuwashia umeme katika banda la VETA wakati wa zoezi la kukagua mabanda kwenye Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (kushoto). 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto),  Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia kwake) wakipata maelezo katika banda la Sido kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini yanayoendelea Mkoani Iringa.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), akikagua gari maalum kwa ajili ya mafunzo katika banda la VETA wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Wanaoshuhudia pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatno kulia). 
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kulia kwake) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza wakikagua vifaa vya mfumo wa umwagiliaji vilivyotengenezwa na VETA katika maadhimisho hayo.
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), akisalimiana na Machifu wa Kabila la Wahehe katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akionesha picha za nyayo za Zamadamu wa Laetoli na Engaresero zilizogundulika Ngorongoro mkoani Arusha takribani miaka milioni 3.6 iliyopita kufuatia tafiti mbalimbali zilizofanyika kwa muda mrefu.
Katika maadhimisho hayo kuna fursa za kuwaona wanyamaori mbalimbali ikiwemo Simba kama wanavyoonekana kwenye banda lao maalum. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad