HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 29, 2017

Ubalozi wa Marekani wazindua kituo cha Kimarekani kuwezesha elimu nchini.

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
Serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania leo imezindua kituo kipya cha kimarekani kitakachokuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia kakinacholenga kukuza fikra yakinifu na mijadala ya kina kuhusu masuala mbali mbali ya kuwapa wananchi haki ya kupata elimu na kupata taarifa bila kikwazo.

Kituo hicho kitakuwa ni daraja la kuzifikia taasisi za elimu ya juu za Kimarekani, taasisi za utafiti, za kimarekani, na hata ufadhili wa masomo na kushirikisha hulka ya ubunifu na ujasiriamali kwa watanzania watakaobuni mustakabali mpya.” Tunawekeza

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kituo hicho, Kaimu balozi wa  Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson amesema, kituo hicho kipya kitakuwa kiunganishi cha kidijitali kati ya Tanzania na eneo la Silicon Valley (kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia)Tehama na ubunifu.

Dk.Patterson amesema Vituo vya Kimarekani ni maeneo yaliyotengwa maalumu katika taasisi mbalimbali za nchini Tanzania “kituo hiki cha lugha ya kiingereza tunachofungua leo kitatoa uwezo wa moja kwa moja wa kujifunza lugha ya Kiingerezaa, ushauri wa elimu, na habari kuhusu fursa za elimu Marekani.

Amesema, kituo hiko kilichopo maktaba kuu jijini hapa kitakuwa wazi kutumiwa na wananchi wote bila malipo oyote na kitakuwa wazi kwa umma kwa siku za Jumatatu hadi Ijumaa na jumamosi asubuhi hadi mchana.

Akifungua kituo hicho, Naibu Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia mhandisi Stella Manyanya amesema, kituo hicho kitakuwa daraja la kuzifikia taasisi za elimu ya juu za kimarekani, taasisi za utafiti na ufadhili wa masomo.

Aidha aliumba ubalozi wa marekani kusaidia kujenga vituo vingine katika mikoa mingi nchini ili kusaidia elimu kwa umma.
 Naibu waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya pamoja na Kaimu balozi wa  Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson wakikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa kituo cha Kimarekani  kilichoanzishwa kwa kushirikiana na Ubalozi wa  Marekani nchini Tanzania pamoja na serikali ya Tanzania.
 Naibu waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya akihutuba katika uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichoanzishwa kwa kushirikiana na Ubalozi wa  Marekani nchini Tanzania pamoja na serikali ya Tanzania. Kituo hicho kitakuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia kitakachowawezesha wananchi kupata elimu na taarifa bila vikwazo. 
 Kaimu balozi wa  Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson akizungumza kuhusu uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichozinduliwa leo kuwa kitakuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia kitakachowawezesha wananchi kupata elimu na taarifa bila vikwazo.
  Mkurugenzi Mkuu wa huduma za maktaba Tanzania, Dk. Alli Mcharazo akielezea faida watakazozipata wananchi kwenye kituo hicho wakati wa uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichozinduliwa leo katika Maktaba ya Taifa jijini Dar es Salaam.

 Afisa Uhusiano wa Ubalozi wa Marekani, Brinille Ellis akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichozinduliwa leo katika Maktaba ya Taifa jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichozinduliwa leo katika Maktaba ya Taifa jijini Dar es Salaam.
  Naibu waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya, akiweka sahihi katika ukuta wa kituo hicho kama ishara ya kumbukumbu ya ufunguzi wa kituo hicho
  Naibu waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya , mwenye suti nyeusi,  Kaimu balozi wa  Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson, katikati na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Maktaba nchini Dk. Alli Mcharazo wakipata maelekezo ya kituo kutoka kwa Afisa wa mambo ya utamadui, Jeff Ladenson.
Naibu waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya, akifurahia jambo kutoka kwenye kitabu kinachopatikana ndani ya kituo hicho, nyuma akishuhudiwa na Kaimu balozi wa  Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson.
 Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi huo.
Picha Avila Kakingo Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad