HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 30 September 2017

Utekelezaji wa awamu ya pili ya Reli ya kati ya kisasa (Standard gauge) waanza Moro-Makutopora

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Prof Makame  Mbalawa  amehudhuria hafla ya kusaini kwa mkataba na mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa reli ya kati ya kisasa itumiayo umeme kwa kiwango cha Standard gauge ambapo itaanzia kipande cha Morogoro hadi Makutopora .
 Hafla hiyo ya utiaji saini ya makubaliano  ya ujenzi  iliyofanyika katika ukumbi wa  Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo kilometa 336 ni za njia kuu na kilometa 86 ni za njia za kupitishia treni na maeneo ya kupangia  mabehewa jumla yake ni kilometa 422 
 Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) inaendeleza  kutekeleza  ahadi za ujenzi wa reli hiyo ikiwa awamu ndogo ya kwanza ujenzi wa  kipande kidogo cha Dar es Salaam hadi Morogoro (KM205) utekelezaji wake umekwishaanza.
Katika utekelezaji  wa awamu ya pili kati ya zile tano  ambazo zinaendelezwa hadi kufikia Mwanza  ujenzi huo una gharimu  takribani  dola za kimarekani 1,923,695,000.
Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Prof Makame  Mbalawa  ameishukuru kampuni ya RAHCO pamoja na Kampuni ya Yapi Merkezi  kutoka nchini Uturuki  kwa kazi kubwa wanayoifanya  katika utelelezaji huo wa awamu ya 1 na ya 2 
  Vile vile Prof. Mbalawa  amepongeza serikali ya awamu ya 5 kwa kuupa  kipaumbele kikubwa mradi huu wa  reli ya umeme kiwango cha Standard gauge ya kisasa, hata hivyo amesema kuwa  kukamilika wa mradi huo ita punguza  gharama za usafiri  kwa wafanyabiashara .
 Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Yapi Merkezi, Erdem Arioglu na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  ( RAHCO) Masanja Kadogosa na Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Yapi Merkezi, Erdem Arioglu wakisaini  mkataba mpya wa ujenzi wa reli mpya ya kisasa ya umeme ya Standard gauge katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) na TRL, Masanja Kadogosa na Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Yapi Merkezi ya Nchini Uturuki, Erdem Arioglu  wakionyesha mikataba  hiyo mara baada ya kumaliza kusaini  leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame  Mbalawa akizungumza  na wageni waalikwa pamoja na kutoa pongezi za dhati kati ya kampuni hizo mbili kwa hatu waliyofikia hadi sasa  makubaliano hayo ya  saini ya ujenzi wa wa reli ya kati kwa kiwango cha Satandard gauge kati ya kampuni ya (RAHCO) pamoja na Yapi Markezi ya Uturuki leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.  Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad