HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 9 September 2017

Picha: Tetemeko kubwa la ardhi laua watu Mexico


Nchi ya Mexico imekumbwa na tetemeko la ardhi linalotajwa kuwa na ukubwa wa nguvu ya 8.1 katika vipimo vya richa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN, limeripoti kuwa tetemeko hilo ambalo limetokea Usiku wa Ijumaa hii wakati watu wamelala limeuathiri zaidi mji wa Mexico City na Guatemala na limesababisha vifo vya watu watano na wengine kujeruhiwa pamoja na kuharibu nyumba na mali za watu.
Rais wa Mexico Enrique Peña Nieto akizungumza na waathirika wa tetemeko la ardhi
Rais wa nchi hiyo Enrique Peña Nieto amesema, tetemeko hilo lilikuwa tetemeko la nguvu zaidi kutokea nchini Mexico katika kipindi cha miaka 100 iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad