HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 5, 2017

MAKAMU WA RAIS AZINDUA TAMASHA LA JINSIA JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Jinsia linalofanyika kwenye viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao Dkt. Vicensia Shule (kushoto) wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la Jinsia lililoandaliwa na TGNP Mtandao. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea tuzo ya Uongozi kwa kuwa Makamu wa Rais wa Kwanza Mwanamke na kutambua mchango wake katika kusimamia na kuhamasisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kutoka kwa mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao Dkt. Vicensia Shule (kushoto) wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la Jinsia lililoandaliwa na TGNP Mtandao.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua Tamasha la 14 la Jinsia lililoandaliwa na TGNP Mtandao
Makamu wa Rais amesema Serikali imechukua hatua mbali mbali ili kumuwezesha mwananke kujikomboa kiuchumi, ikiwa pamoja na kuanzisha Benki ya Wanawake Tanzania, kuanzisha mifuko mbali mbali ya uwezeshaji ukiwemo mfuko wa Maendeleo ya Wanawake pamoja na kuhamasisha uanzishwaji wa SACCOS na VICOBA na vikundi vingine vya kiuchumi pia serikali iliagiza Asilimia 30 ya zabuni za serikali zipewe wanawake, vile vile iliagiza halmashauri zote kutenga asilimia 5 ya mapato kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake.
Alisema “ Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini umuhimu wa uzingatiaji wa masuala ya jinsia katika kuchangia na kuharakisha  maendeleo ya nchi”.
Mhe. Samia alitoa wito kwa wadau wa maendeleo  kushirikiana katika kuhakikisha Tanzania kama nchi tunafikia lengo namba 5 la ajenda ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya mwaka 2063 ya Afrika ya kuhakikisha Mwanamke ana haki sawa na mwanaume katika Nyanja zote za kijamii na haachwi nyuma kwenye maendeleo.
Makamu wa Rais alisisitiza ni muhimu kwa Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuzingatia vipaumbele vya kijinsia kwenye mipango yake ya bajeti.
Makamu wa Rais alisema ili kufikia usawa wa kijinsia lazima mwanamke apewe mbinu za kumuezesha kiuchumi na lazima alindwe  na vitendo vya ukatili wa kijinsia ili aweze kusimama imara kwenye majukumu yake mbali mbali.
Makamu wa R­­ais alihimiza pia Wanawake kusaidiana na kuinuana ili kufikia malengo .
Mwisho Makamu wa Rais aliwapongeza TGNP na Kamati ya Kitaifa ya kuweka kumbukumbu za wanawake kwa ajili ya kuwatambua, kuwaenzi na kuweka kumbukumbu za michango ya wanawake katika nyanza mbali mbali za maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad